WAZIRI PROF MBARAWA, AITAKA SUMATRA KUDHIBITI AJALI
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Kikwetu
Mkoani Lindi Bw. Boniface Njanda (Wa kwanza Kulia) wakati alipotembelea
uwanja huo.
Meneja
wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Lindi Eng. Isaac
Mwanawima akitoa taarifa ya utendaji wa Wakala huo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto)
wakati alipotembelea wakala huo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) mkoa wa Lindi Eng.
Hillary Msaki, wakati alipotembelea wakala huo,mkoani Lindi.
Mtaalam
wa ufundi na Mitambo wa Kampuni ya Simu nchini (TTCL) akifafanua jambo
kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
namna ya Mitando ya TTCL inavyofanya kazi, Mkoani Lindi.
Kaimu
Meneja wa Bandari ya Mtwara Bi. Stella Katondo akitoa taarifa ya
maendeleao ya upanuzi wa bandari ndogo ya Lindi kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Mwenye shati nyeupe),
wakati alipokagua ujenzi huo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na
wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Mkoani Lindi.
Mmoja
wa wafanyakazi wa Shirika la simu Tanzania (TTCL) akitoa maoni yake kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
alipoongea nao Mkoani Lindi.
Mratibu
wa Huduma za Posta mkoa wa Lindi Bw. Dominick Kalangi akimuelezea
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa
pili kushoto) kuhusu huduma za barua na vifurushi vinavyopokelewa na
kusafirishwa sehemu mbalimbali za nchi.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua
huduma za mtandao katika moja ya ofisi za Shirika la Posta (TPC) Mkoani
Lindi.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo ya kuzingatia viwango kwa mkandarasi wa Kampuni ya Comfix
& Engineer Eng. Robert Lupinda (Wa kwanza kulia) anayejenga Bandari
ndogo ya Lindi.
……………………………………………………………………………………….
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameutaka
uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(SUMATRA) kutoa adhabu kali kwa wamiliki wa vyombo vya usafirishaji na
madereva wazembe wanaosababisha ajali za barabarani.
Ameyazungumza
hayo wakati wa ukaguzi wa utendaji kazi kwa wafanyakazi wa taasisi
zilizopo chini ya Wizara hiyo pamoja na miundondombinu ya Barabara,
Bandari, Mawasiliano na kiwanja cha ndege cha Kikwetu mkoani Lindi.
Profesa
Mbarawa amesema kuwa ongezeko la ajali zinazosababisha vifo kutokana na
uzembe wa madereva, kutofuata sheria na alama zinazowekwa barabarani
zizidhibitiwe ili kuokoa maisha ya watanzania na nguvu kazi ya Taifa.
“Nataka
kuona wamiliki wa vyombo vya usafiri na madereva wazembe wanaposabisha
ajali na kuua watu wanafutiwa leseni zao vile vile nawataka mfikirie
kwanini watanzania wengi wanaendelea kufa kwa ajali za barabarani ili
muweze kutafuta ufumbuzi wa namna ya kudhibiti ajali hizo”, amesisitiza
Prof. Mbarawa.
Katika
hatua nyingine Waziri Mbarawa amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Eng. George Sambali kukamilisha kazi
ya kupima eneo la kiwanja cha Kikwetu ili kupata hati miliki na
kudhibiti uvamizi wa kiwanja hicho
“Kama
kiwanja hiki hakitapimwa watu watavamia eneo la kiwanja na Serikali
italazimika kuingia gharama za kulipa fidia hivyo kuchelewesha maendeleo
ya uwanja huo”, amesema Prof. Mbarawa.
Ameongeza
kuwa Serikali iko kwenye hatua za mwisho za kutafuta fedha kwa
kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ili kuimarisha
miundombinu ya kiwanja hicho na kuongeza chachu ya maendeleo Mkoani
humo.
Naye
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Kikwetu, mkoani Lindi Bw. Boniface Njanda
amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa Mamlaka itafanya tathmini ya
Kiwanja hicho kabla ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.
Waziri
Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua utendaji kazi kwa wafanyakazi wa
taasisi zilizopo chini ya Wizara na kuangalia maendeleo ya utekelezaji
wa miradi katika kanda ya kusini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments