WASHINDI WANNE WANYAKUA ZAWADI KATIKA KAMPENI YA FAIDIKA NA AMANA BANK
Mkurugenzi
wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi ya Television
mshindi wa kwanza wa kampeni ya Faidika na Amana Bank Bi PIKIRA NLONGANE
wakati wa Hitimisho la kampeni hiyo iliyokuwa na lengo la kuwajengea
uwezo watanzania wa kuwekeza zaidi,Hitimisho la Kampeni hiyo limefanyika
wakati wa siku ya maonyesho ya kimataifa ya biashara saba saba Jijini
Dar es salaam ambayo Bank ya amana ni moja kati ya wafanyabiashara
waliokuwa na Banda katika Maonyesho hayo
|
Zawadi
ya JOKOFU kwenda kwa mshindi wa pili ambaye ni SHAKIRA IBRAHIMU
imekabidhiwa na kupokelewa na mwakilishi wake ambaye ni AHMED SANDE
(Pichani) akikabidhiwa zawadi hiyo na Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR
MUHSIN MASOUD wakati wa utoaji wa zawadi hizo.
|
Mshindi
wa nne amepata zawadi ya Table Feni ya kisasa yenye AC pia.Pichani
ni Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi
Bwana HEMED SULEIMAN ambaye ameibuka mshindi wa nne katika kampeni ya
Faidika na Amana Bank iliyochezeshwa ndani ya banda la Bank hiyo katika
maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya saba saba Jijini Dar es salaam
ambapo washindi wanne wamejinyakulia zawadi mbalimbali zenye thamani ya
shilingi za kitanzania Million Tano
|
Mkurugenzi
wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akizungumza na wanahabari wakati wa
Utoaji wa zawadi hizo kwa washindi wanne wa Kampeni ya Faidika na Amana
Bank ambapo amewataka watanzania kuwa na utamaduni wa kuwekeza kwani ni
utamaduni mzuri na unaofaa kuendelezwa
Katika kuadhimisha kilele cha kampeni ya FAIDIKA NA AMANA BANK,Bank imezawadiwa wateja wake waliobahatiika kushinda zawadi mbalimbali kutokana na kujiwekea akiba zao na Benk hiyo leo siku ya kilele cha maonyesho ya saba saba
Amesema Wateja
hao walichaguliwa kitaalam katika droo iliyochezeshwa ndani ya viwanja
vya saba saba katika banda la amana bank na kupewa taarifa ya kufika
kupokea zawadi zao kutoka uongozi mkuu wa bank hiyo wakiongozwa na
Mkurugenzi mtendaji DR MUHSIN SALIM MASOUD.
Kampeni
hiyo iliyojumuisha wateja wa akaunti za akiba binafsi kujiwekea akiba
katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi 500,000 na kuendelea kwa
muda wa miezi mitatu na kuweza kupata nafasi ya kujishindia zawadi
mbalimbali za vifaa vya matumizi ya nyumbani kama
Luninga,Jokofu,Microwevu,
|
Meneja
masoko wa Bank ya Amana Ndugu DASSU MUSSA akifafanua jambo kwa
wanahabari ambao walifika kushughudia Utoaji wa zawadi hizo katika Banda
lao lililopo katika maonyesho ya saba saba ambayo ndiyo yanaelekea
ukingoni
Akizungumza
na wanahabari mapema leo wakati wa utoaji wa zawadi hizo kwa washindi
hao meneja masoko wa Bank hiyo Ndugu DASSU MUSSA amesema kuwa bank ya
amana imejipanga kuendelea kuwafikia na kuwapatia watanzania wote huduma
bora zenye ubunifu na zenye tija kufuatana na mahitaji yao
mbalimbali,huDuma pia ambazo zinafwata misingi ya sheria ya kiislamili
kuwapatia faida iliyo halali na kuwaondoa katika mzigo wa riba.
Aidha
amewahamasisha watanzania wote kujijiengea na kudumisha utamaduni wa
kujiwekea akiba ya pesa kwa ajili ya malengo mbalimbali katika benk ya
amana ili wapate kufurahia huduma bora zitowelewazo kwa ufanisi na
weledi wa hali ya juu.
|
Ameongeza
kuwa kampeni ya faidika na amana bank ni mwanzo tu wa kampeni za bank
hiyo zitakazohusisha wateja kuweka fedha na kujishindia zawadi
mbalimbali kutoka amana bank ukiachia faida nyingine zipatikanazo kwa
wateja kujiwekea akiba huku akisema kuwa wanatarajia kutangaza kampeni
nyingine kubwa itakayowezesha wateja wengiine Zaidi kujishindia zawadi
lukuki kutokana na kujiwekea utaratibu wa kuweka akiba zao amana Bank
Bank ambayo inafwata misingi ya kiislam kikamilifu.
Zawadi ambazo zimetolea kwa washindina Bank ya Amana ambazo jumla zimegharimu kiasi cha shilingi million Tano
|
Aidha
akiwahamasisha watanzania kujiunga na Bank hiyo amesema kuwa watanzania
wengi wamekuwa wakidhani Bank hiyo ni kwa ajili ya waislam jambo ambalo
sio kweli huku akitanabaisha kuwa Bank hiyo inahusisha wateja wa Dini
zote bila kubagua hivyo watanzania wajiunge kwa wingi katika Bank hiyo,
Washindi
waliojishindia zawadi mbalimbali katika hitimisho la Kampeni hiyo ya
Faidika na Amana Bank ni pamoja na Pikira Nlongane aliyejishindia zawadi
ya Televission kwa kuwa mshindi wa kwanza,Shakira Ibrahim aliyeshika
nafasi ya pili na kujishindia zawadi ya Friji kubwa,Khamis Said
aliyejishindia Microwave huku mshindi wa nne akiwa ni Hemed Suleiman
aliyejishindia Table Feni katika droo hiyo.
Picha
ya Pamoja maafisa wa Bank ya amana wakiwa na washindi wa Zawadi
mbalimbali za kampeni ya Faidika na Amana Bank mara baada ya utoaji wa
zawadi hizo katika maonyesho ya Saba saba
|
Bank
ya amana ni bank inayoongozwa kwa ustadi mkubwa na misingi ya Dini ya
kiislam huku ikiwahudumia watanzania wapatao Elfu 34 katika matawi yake
saba nchi nzima hadi sasa.
PICHA NYINGINE ZAIDI WATEJA WAKIMIMINIKA KATIKA BANDA LA AMANA BANK KATIKA MAONYESHO HAYO
No comments