VIJANA WAASWA KUJIAJIRI KUPITIA FILAMU.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Bibi. Venorose Mtenga akizungumza na vijana kuhusu umuhimu wa kujiajiri kupitia ujasiliamali katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana Julai 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo akitoa mada kuhusu umuhimu wa sekta ya filamu kwa vijana katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana kuhusu vijana kujiajiri kupitia sekta ya filamu Julai 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Hafidhi Omary akichangia mada katika mafunzo kuhusu umuhimu wa kujiajiri kupitia ujasiliamali na filamu katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana Julai 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Zuhura Madaba akichangia mada katika mafunzo kuhusu umuhimu wa kujiajiri kupitia ujasiliamali na filamu katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana Julai 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Inspekta Athuman Mtasha akichangia mada katika mafunzo kuhusu umuhimu wa kujiajiri kupitia ujasiliamali na filamu katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana Julai 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vijana wakifatilia mafunzo kuhusu umuhimu wa kujiajiri kupitia ujasiliamali na filamu katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana Julai 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Shamimu Nyaki-WHUSM)
……………………………………………………………………………………………………
Na Shamimu Nyaki WHUSM.
Serikali imewaasa Vijana nchini
kujiajiri kupitia filamu kwakua ni Sekta ambayo inatoa nafasi kubwa kwa
kundi hilo lenye uhitaji mkubwa wa ajira hapa nchini.
Wito huo umetolewa jijini Dar es
Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo alipokuwa
akitoa mafunzo kwa Vijana kuhusu Umuhimu wa Sekta ya Filamu katika kutoa
ajira kwa vijana.
Amesema kuwa Sekta ya Filamu ni
Sekta ambayo inaweza kusaidia vijana kujiajiri kwa kuwa ina vipengele
vingi vinavyoweza kuwasaidia ikiwemo uandishi wa Mswaada, utengenezaji
wa Filamu, uigizaji, upigaji picha na kuhariri.
“Takribani asilimia 70% ya watu
wamepata ajira kupitia filamu hivyo ni vyema na nyie mkatumia elimu
mnayopata hapa na vipaji vyenu kufanya filamu ili kujikomboa
kiuchumi”Alisema Bi Joyce.
Ameongeza kuwa ni vyema Vijana
kuwa wazalendo kwa kutengeneza Filamu ambazo zitakuwa na maadili ya
kitanzania ambazo zitakuwa zinatazamwa na kila mtu bila kujali umri
kwakua Filamu mbali ya kuelimisha pia inatoa burudani.
Aidha Kijana Hafidh Omary
ameishukuru Bodi ya Filamu kwa elimu iliyotoa kwa vijana hao ambapo
wameweza kujua mambo mengi kuhusu Filamu ikiwemo hatua gani za kufuata
kabla ya kutengeneza Filamu ili kuepuka kutoa filamu ambayo haiwezi
kupata kibali kutoka Bodi ya Filamu.
“Binafsi namshukuru Katibu
Mtendaji kuanzia sasa najua kuwa kabla ya kufanya filamu lazima kwanza
niende Bodi ya Filamu nikapewe kibali na baada ya kutengeneza filamu
yangu niirudishe tena katika ofisi hizo ili ikakaguliwe niweze kutoa
Filamu bora na yenye Madili”. Alisema Bw Hafidh.
Hata hivyo Bodi ya Filamu ina
lengo la kuwasadia vijana kujifunza zaidi ambapo inatarajia kuwapeleka
watu thelathini nchini Nigeria kujifunza zaidi filamu ili kuinua soko la
hapa nchini kwa wasanii wa filamu.
No comments