VIJANA MKOANI DAR WAJIANDIKISHA MASOMO YA VETA KUPITIA VSOMO YA SIMU ZA AIRTEL
Ikiwa
ni takribani mwezi moja tangu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa
kushirikiana na VETA kuzindua application ijulikanayo Kama VSOMO na
kuwawezesha watanzania kusoma masomo ya ufundi kupitia simu zao za
Mkononi.
Airtel
na VETA imeendelea kutoa elimu kwa vijana na wakazi wa Dar katika
maonyesho ya sabasaba ili kuhakikisha Taarifa taarifa muhimu kuhusu
mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu zinawafikia watanzania wengi na
kuwanufaisha vijana nchini kujisomea na kuongeza ujuzi.
Mpaka
sasa zaidi ya vijana 700 mkoani Dar Es saalam wameshajiandikisha na
Kati yao wameshaanza kusoma kozi mbalimbali Kwa maelezo zaidi kuhusu
VSOMO tuandikie kupitia airtelfursa@tz.airtel.com
Mabalozi
wa Airtel Tanzania wakitoa maelezo kwa wateja waliotembelea banda la
Airtel, juu ya mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao
za mikononi ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana
na Airtel kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea
kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa Airtel Tanzania, Emmanuel Alfred akitoa maelezo juu ya mpango mpya
wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mikononi ujulikanayo kama
VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana na Airtel kwenye Maonesho ya
40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Chuo cha Ufundi Veta Kilichopo Kipawa Jijini Dar es salaam,Mhandisi
Lucius Lutenganya akitoa maelezo kwa waliotembelea banda la VETA juu ya
mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mikononi
ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana na Airtel
kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye
Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa Mradi wa VSOMO Tanzania Gosbert Kakiziba kutoka VETA Kipawa Jijini
Dar es salaam akitoa maelezo kwa waliotembelea banda la VETA juu ya
mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mikononi
ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana na Airtel
kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye
Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhitimu
wa Kozi ya umeme Salehe Shomari, akitoa maelezo kwa waliotembelea banda
la VETA juu ya mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao
za mikononi ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana
na Airtel kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea
kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
No comments