Breaking News

URENO YATANGULIA FAINALI YA EURO 2016,YAILAZA WALES 2-0

Ulikuwa mtanange wa kukata na shoka wa nusu fainali ya michuano ya Euro 2016 inayotimua vumbi kule nchini Ufaransa kati ya Wales iliyokuwa ikiongozwa na Gareth Bale na Ureno ikiongozwa na Christian Ronaldo.
 
Mtanange huo ulio kanyagwa katika dimba la Parc de Olimpique jijini Lyon, ulichezeshwa vizuri na mwamuzi Jonas Eriksson wa Sweden na mpaka mapumziko timu hizo hazikuweza kufungana ingawa kila timu ilitengeza nafasi kadhaa za kuweza kujipatia mabao laikn umaliziaji ukawa mbovu.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi zaidi na walikuwa Ureno wlianza kuhanikiza ushindi,si mwingine bali ni Christian Ronaldo kunako dakika ya 50 yaani dakika 5 tu baada ya kuanza kipindi hicho anafunga bao zuri kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona fupi toka kwa Guerreiro.

Na dakika 3 baadaye Ronaldo anapiga shuti kali langoni mwa Wales akiwa umbali wa mita 25 na mpira huo unawapita walinzi wa Wales ambapo Luis Nani wa Ureno anaserereka na kuuunganisha wavuni akiianikia timu yake bao la pili.

Kuona jahazi linazama kocha wa Wales Chris Coleman anamtoa Joe Ladley na kumwingiza Sam Vokes huku akibadili mfumo toka 3-5-1-1 na kucheza 4-3-1-2,lakini hiyo haikusaidia kubadili matokeo mbele ya Ureno waliokuwa wakicheza mfumo wa 4-1-3-2.
Sasa Ureno anamsubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya wenyeji Ufaransa na Ujerumani kucheza naye fainali siku ya jumapili Julai 10 2016 katika dimba la Stade de France,Paris.

No comments