UCHUNGUZI UNAENDELEA KUBAINI BAWA LA NDEGE LILILOOKOTWA NA WAVUVI KATIKA KISIWA CHA KOJANI PEMBA
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga
Tanzania imesema uchunguzi wa kitaalamu bado unaendelea ili kubaini
iwapo bawa la ndege lililookotwa na wavuvi katika Kisiwa cha Kojani
Pemba ni mabaki ya ndege ya Malyasia .
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo
Vallery Luanda Chamlungu ameyabainisha hayo wakati wa makabidhiano ya
bawa hilo yaliyofanyika katika bandari ya Kojani na kushuhudiwa na
Viongozi wa mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya
Wete .
Alisema , pamoja na uchunguzi wa
kitaalamu unaofanywa na mamlaka hiyo , lakini pia Uongozi unaendelea
kuwasiliana na mashirika ya ndege ya kimataifa ya ili kusaidia
kukamilisha machakato wa kutambua asili ya ndege hiyo .
“Uchunguzi bado unaendelea ili
kubaini kwamba bawa hilo ni mabaki ya ndege ya Malyasia iliyopotea miaka
kadhaa iliyopita , tunafanya mawasiliano na mashirika ya ndege ya
kimataifa na hili bawa tunatarajia wenzetu kutoka Malyasia watakuja
”alifahamisha Chamlungu .
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo
alisema wataendelea kushirikiana na wananchi kufanya utafiti hasa
sehemu za baharini sambamba na kuwashukuru wavuvi wa Kojani kwa kuweza
kulihifadhi bawa hilo .
Aidha , Mkuu wa Wilaya ya Wete
Rashid Hadid Rashid akikabidhi bawa hilo aliwataka wananchi
kuwasiliana na vyombo vya ulinzi wanapookota vitu baharini , na kuacha
kuvihifadhi majumbani kwani baadhi vinaweza kuwa ni hatari kwa maisha
yao .
Alisema , Serikali ya Wilaya
ilisimamia ili kuona kwamba bawa hilo linahifadhiwa , na linabaki
katika mazingira yaliyo salama ili kupisha uchunguzi wa kitaalam
ufanyike .
“Pamoja na juhudi zenu , lakini
pia naomba nitoe wito kwa wavuvi kutoa taarifa Serikalini ili kuepisha
utokea kwa madhara yasiyotarajiwa , baada ya kuhifadhi majumbani mwenu ”
alisisitiza Mkuu wa Wilaya.
Mmoja wa mashuhuda waliookota
bawa hilo Chungua Hamad Chungua aliishauri mamlaka ya Usafiri wa Anga
kuwaandalia mazingira mazuri ya kuwapatia mashine ya uvuvi ambayo
itawasaidia katika kazi zao za uvuvi .
Alisema , ni vyema Mamlaka hiyo
kuwazawadia mashine ya supa kumi au kumi na tano kutokana na usumbufu
walioupata wakati wa kulikokota kwani ni zito na bahari ilikuw
aimechafuka .
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Usafiri wa Anga iimekabidhi shilingi milioni mbili wavuvi
waliofanikisha kuliokota na kulihifadhi kama ni zawadi .
Kwa mujibu wa taratibu na sheria
, Mamlaka ya Usafiri wa Anga haina ulazima wa kuwalipa wananchi
wanaokota vitu aidha baharini au nchi kavu , isipokuwa hulazimika kutoka
zawadi ili kuwajenga imani wananchi ya kuvihifadhi vitu wanavyo viokotaNa Masanja Mabula –Pemba
No comments