Breaking News

DK, MPANGO AWATAKA WANANCHI KUNUNUA HISA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI


                          Waziri wa fedha na uchumi Dk.Philip Mpango


Serikali imewataka wananchi kujenga utamaduni wa kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwa kuwekeza na  kununua hisa zinazouzwa na soko la hisa la Dar es salaam (DSE) Ili kuondokana na umasikini wa kipato.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Waziri wa fedha na uchumi Dk.Philip Mpango amesema kuwa hili  nchi iweze kufifikia uchumi wa kati ni lazima wananchi washiriki katika shughuli za uzalishaji mali na kuwekeza mitaji yao kwa kununua hisa zinazo uzwa na soko la hisa la Dar es salaam.

Amesema  nchi yoyote duniani wananchi ili waweze kukua kiuchumi ni lazima wananchi hao kushiriki katika shughuli za kiuchumi pamoja na kujenga mazoea ya ununuzi wa hisa.
Dk  Mpango ameongeza kuwa ushiriki wa wananchi katika ununuzi wa hisa kutawezesha wananchi kuwa wamiliki wa makampuni mbalimbali nchini hali itakayowawezesha kuondokana na umasikini wa kipato .

Amesema watanzania ipo haja ya kuangalia fursa za kuwekeza hasa katika masoko ya mitaji pamoja na makapuni yaliyo binafsishwa kwa kununua hisa katika makampuni hayo ili  kushiriki katika kujenga uchumi .

Aidha Dk Mpango ameongeza kuwa wananchi wajitokeze kwa wingi kulitumia zaidi soko la hisa kwajili ya kufanya ununuzi wa hisa katika makampuni mbalimbali hili kujiletea maendeleo zaidi na kuweza kuboresha mitaji yao.

No comments