TANZANIA DISTILLERIES LIMITED (TDL) YAZINDUA KAMPENI YA NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI KWA WASAMBAZAJI WAKE NCHINI
Meneja Masoko na Udhamini wa TBL
Group,George kavishe akiongea na baadhi ya mawakala wakati wa
uzindinduzi wa kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji
wa bidhaa zake .Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika ukumbi wa Protea
jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa mawakala wa kampuni ya
Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL), Bi.Grace Ulomi
akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi
Meneja Masoko na udhamini wa TBL
Group, George Kavishe akiongea na waandishi wa habari wakati wa
uzindinduzi wa kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji
wa bidhaa zake .Wengine pichani ni Maofisa wa kampuni hiyo.
Baadhi ya mawakala waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo.
Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayotengeneza
na kusambaza kinywaji maarufu cha Konyagi na jamii zake, leo imezindua
rasmi kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa
zake itakayodumu kwa muda wa wiki 12.
Akizungumza katika uzinduzi wa
kampeni hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Protea Oystebay – Dar es
salaam, Mwakilishi wa Kampuni ya TDL, Meneja Masoko na Udhamini Bwana
George Kavishe alisema; “Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL kuzindua
kampeni ni kwanza kabisa kuwainua wasambazaji wa biashara zetu. Tutaweza
kufikia lengo hili kwani washindi wa kampeni hii watajishidia magari
mapya mawili ya usambazaji (Eicher 3 Tonne Truck). Tunaamini kwa magari
haya wasambazaji wetu wataweza kurahisishwa utendaji wao ndani ya maeneo
yao ya mauzo”
Pia, kupitia shindano hili tutaweza kuchangia maendeleo ya kichumi nchini pamoja na jamii kwa ujumla. Aliendelea kusema.
Naye Meneja Mkuu wa TDL; Devis
Deogratius alisema “Katika shindano hili wasambazaji wa bidhaa zetu
wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo
wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi baada ya miezi 10.
Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao
watoongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.
No comments