MA DJ WATAKIWA KUJISAJIRI ILI KUIMARISHA TAALUMA YAO
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni , Sanaa na Michezo akikabidhi vyeti vya
usajili wa Chama cha Madijey nchini leo jijini Arusha kwa Mwenyekiti wa
Chama hicho Bw.Yusuph Juma kuashiria uzinduzi wa chama hicho rasmi.
Naibu
waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wmbura akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya madijey waliyo wanachama mara baada
ya kuzinduliwa kwa chama hicho leo jijini arusha,(wanne kulia) ni
Katibu tawala Mkoa Bw.Hargeney Chitukuro
…………………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO-Arusha.
Wasanii wa wanofanya kazi ya u-dijey watakiwa kujisajili katika Chama kwa lengo kujenga misingi imara ya taalum hiyo.
Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha
na Naibu Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo alipozindua chama
hicho rasmi katika mkutano wa wadau wa kisekta uliyofanyika katika
ofisi za Mkuu wa Mkoa ambapo alikutana na wadau mbalimbali.
“Kuanzishwa kwa chama hiki
kuanashiria ni kwa kiasi gani wadau wa sekta ya sanaa wameelewa umuhimu
wa kurasimisha kazi zao na hili litaongeza tija katika kujenga heshima
ya kada hii ya madijey katika nchi yetu kama ilivyokwa nchi
zilizoendelea”,alisema Naibu Waziri Wambura.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama
cha Madijey Bw.Yusuph Juma alisema wameamuo kuanzisha chama hicho cha
madijey kwa kuwa sanaa hiyo imekuwa ikidharaulika kwa kiasi kikubwa
imekuwa ikionekana kama siyo sekta rasmi bali ni uhuni .
“Usajili wa madijey katika chama
utazingatia vigezo vya taalum pamoja na leseni za udijey hii ni kwa
lengo la kuimarisha sekta hii ili kuipa nguvu na kuifanya iheshimike
kama kazi nyingine za kisana na sivinginevyo”,alisema Bw.Juma.
Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo
alisema madijey wengi nchini wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa kulipwa
ujira mdogo ukilinganisha na masaa wanayokuwa wakifanya kazi
hiyo,hivyo kwa kupitia umoja huo wataunda muongozo utakaosaidia
kuboresha mazingira ya malipo yao.
Pia Bw.Juma ameiomba serikali
kusimamia suala la madijey wote nchini kujiunga katika chama hicho kwa
lengo la kuunda umoja wao utakowasaidia kupata fursa mbalimbali za
kimaendeleo ikiwemo kutafuta namna ya kuongeza maslai yao.
Hata hivyo uongozi huo umetoa
shukrani kwa Serikali kwa ushirikiano uliyowapa katika kupitisha chama
hicho ambacho kimesajili katika Baraza la Sanaa la Taifa .
No comments