SHEIKH JALALA AMEONGOZA WAISLAM NA WAUMINI WA DINI MBALIMBALI MATEMBEZI YA AMANI YA SIKU YA KIMATAIFA YA QUDS DAR
Kiongozi
mkuu wa dhehebu la shia Ithnasheriya Sheikh Hemed Jalala amewaongoza waislam na
waumini wengne wa wa dini mbalimbali katika matembezi ya amani ya siku ya
kimataifa ya kupinga manyanyaso,dhulma na mateso dhidi ya wapalestina
yanayofanyika kila ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
Akizungumza
na umma wa washiriki wa matembezi hayo shekh jalala amesema zaidi ya karne na
karne sasa tangu dunia ianze kushuhudia mapigano na mgogoro kati ya wa Israel
na Palestina juu ya umiliki wa ardhi ya taifa la Palestina, pamoja na jitihada
za kuutatua mgogoro huo ikiwemo kurekebisha mipaka ya ardhi kushindwa kufikia
muafaka..
Amesema
ili dunia iwe na amani na mahala salama pa kuishi, ni lazima kuitetea na kuunga
mkono mapambano dhidi ya unyanyasaji, dhulma na uonevu dhidi ya wapalestina
kama alivyofanya Hayati Mwalimu Nyerere na Nelson Mandela kwa kukemea
yanayotokea katika adhi ya palestina kwa kipindi kirefu kwani leo yapo
Palestina ila kesho huenda yakaenea ulimwengu mzima.
Matembezi
ya mwaka huu yamebeba ujumbe
“Tuwaonee huruma Wapalestina”
No comments