Sheikh mkuu wa mkoa wa dar es Salaam, Alhadi salum Mussa akifafanua jambo
katika semina ya siku ya quds iliyofanyika jijini dar es Salaam katika ukumbi
wa karimjee.
Akiwasilisha mada katika semina ya siku ya QUDS jijini dar, Shekh
Alhadi Salum Mussa amesema anaunga
mkono harakati za kuwafanya wazawa wa palestina kuwa huru na wenye kuishi kwa
amani.
Amesema suala la maisha
ya wananchi wa palestina ni swala la kuungwa mkono na kila mpenda haki bila
kujali itikadi za kidini ilo ni jukumu la kila mwanadam kusimama kupaza sauti
kukemea dhulma yanayotokea katika ardhi ya palestina.
Aidha Alhadi Mssa ameongeza kuwa kila tarehe 1/7 dunia inaazimisha
siku quds, siku ambayo inaazimishwa kila mwaka kwa lengo kupaza sauti kukemea
mateso wanayoyapta wananchi wa palestina katika ardhi yao kwani sio swala la
kuvulika hata kidogo.
|
No comments