Breaking News

DK. KIKWETE KUPEWA TUZO YA AMANI NCHINI.

Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kupewa tunzo ya amani itakayotolewa na Taasisi ya Maridhiano ya Tanzania julai 13 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Taasisi ya Maridhiano nchini Bw,Sadick Godi Godi amesema sambamba na kutoa tuzo hiyo ya amani kwa Rais Kikwete, pia taasisi hiyo inatarajiwa kutoa tuzo kwa Mama Maria Nyerere kwa mchango wake katika taifa la Tanzania kama Muasisi wa taifa la Tanzania na mdau wa amani.

Amesema Rai Mstaafu Kikwete atapewa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake katika kuleta utengamano wa amani hasa katika nchi mbalimbali ikiwemo kutatua migogoro katika nchi za Burundi na Rwanda.

Amewataja wengine ambao katika halfa hiyo watapewa tuzo hiyo ya amani kuwa ni Mkuu wa jeshi la polisi Mstaafu Said MWEMA ambae amemwelezea pia kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kusimamia amani kwa kuanzisha polisi jamii nchini.

Aidha bw Godi Godi amesema taasisi hiyo pia inatambua mchango wa Mwenyekti wa makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi kama mtu muhimu katika kusaidia makundi maalum ya watu hasa wenye ulemavu.

Amewataja wengine ambao watapewa tuzo kwa kutambua mchango wao kwa jamii au kwa nchi siku hiyo kuwa ni mfanyabiashara maarufu jijini bw Sabodo atapewa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake  kwa mchango wake katika kuisaidia jamii hususani uchimbaji wa visima.

Wengine ni Bi, Hellen Kijo Bisimba mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu kwa mchango wake katika kupigania haki za binadam nchini, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Sadick Mecksadick, Mkurugenzi wa Clouds Media bw Ruge Mutahaba, Mwanzilishi na Spika wa bunge la uchumi Tanzania Bw Albert Sanga pamoja na Mbunge wa jimbo la segerea mhe,BONA kaluwa.

No comments