Ukuaji wa Sayansi na Teknolojia umekuwa
na faida na changamoto zake licha ya kurahisisha ufanyikaji wa shughuli
mbambali ikiwa ni moja ya faida lakini kumekuwa na changamoto ikiwemo
kwenye sekta ya mawasiliano ambapo kumekuwa na uhalifu mkubwa na
kupelekea upotevu wa fedha katika mitandao huku ikiripotiwa kuwa
kumekuwa na upotevu wa Dola za Kimarekani Bilioni 300 kila mwaka
kutokana na wizi wa kimtandao.
Hivyo Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano kupitia Sekta ya Mawasiliano kwa kushirikiana na Oracle
Corporation wameandaa Mkutano maalumu ambao wa Cyber Security Summit in
Africa unaotaraji kufanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Kilimanjaro
ukiwa umelenga kutatua changamoto za uhalifu wa kimtandao.
Akizungumza na jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Shirika hilo Race Region amesema kuwa Mkutano huo
mkubwa kwa bara la Afrika unatarajia kufanyika Tanzania kwasababu ni
moja ya nchi ambayo imepiga hatua kwenye masuala ya Tehama hata Rais
Magufuli amekuwa akiunga mkono jitihada hizo na kuagiza ukusanyaji wa
kodi kwa njia ya Kielektroniki, huku akiongeza kuwa wameambatana na
wataalamu wa masuala ya mtandao kutoka nchi mbalimbali ambao watawapa
mbinu za namna gani wameweza kudhibiti suala la wizi wa kimtandao katika
nchi zao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi idara
ya Tehama Wizara ya Uchukuzi Ujenzi na Mawasiliano katika Sekta ya
Mawasiliano Shabani Pazi amesema kuwa serikali inajitahidi kudhibiti na
kuboresha sekta hiyo kwani imejenga mkongo wa Taifa karibu mikoa yote na
inampango wa kuzifikia wilaya zote nchini, pia serikali imejenga kituo
cha Data ambacho kinatumika kuhifadhi taarifa mbalimbali kwa usalama,
vilevile serikali imeweza kuweka sheria ya Miamala na Makosa ya
Kimtandao (Cyber Crime Act) ya mwaka 2015 ambazo zinaendelea kudhibiti
uhalifu wa kimtandao.
Picha; MOSHI SHABANI
MKUTANO MAALUMU WA CYBER SECURITY SUMMIT IN AFRICA KUFANYIKA JIJINI DAR KESHO
Reviewed by Harakati za jiji
on
June 29, 2016
Rating: 5
No comments