TUWAKOMBOE WAPALESTINA; SHEIKH JALALA:
Kiongozi mkuu
wa waislam wa dhehebu la shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala ametoa wito
kwa watanzania wa dini zote kujitokeza kushiriki matembezi ya amani yatakayofanyika
siku ya tarehe 1/7 jijini dar Es Salaam kupinga dhulma,unyanyasaji,uonevu unaondelea
kwa watu wa Palestina kama ishara ya kutokuunga mkono na kukemea kinachofanyika
katika ardhi ya palestina.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam amesema matatizo wanayo yapata wapalestina ni makubwa na kwamba leo hii sio ajabu kuvunjiwa nyumba zao za ibada, Watoto kukosa haki zao za msingi pamoja wanawake kujifungulia kwenye vizuizi njiani na kubwa zaidi ni kushambuliwa na kuuliwa bila hatia.
Sheikh
Jalala ameongeza kuwa ili dunia iwe na amani na mahala salama pa kuishi ipo
haja ya kutetea na kuunga mkono mapambano dhidi ya unyanyasaji, dhulma na
uonevu dhidi ya wapalestina kama alivyofanya Hayati Mwalimu Nyerere na Nelson
Mandela kwani yanayotokea leo Palestina, huenda yakaenea ulimwengu mzima katika
dhana ya imani za kidini.
Nae
mjumbe wa kamati ya mandalizi ya matembezi hayo Profesa abdul sharif amesema dunia nzima inatakiwa
kukemea kwa nguvu kinachotokea nchini palestina pamoja na kukiuka haki za
binadamu kinawakosesha haki za msingi mbalimbali nchini humo.
Kwa upande
wake bi Nice Munissy akitoa ushuhuda wa hali alioshuhudia nchini palestina
amesema wananchi wa palestina wanatakiwa kuungwa mkono kwa kupaza sauti
duniani kote kukemea yanayotokea katika ardhi ya nchi hiyo kwani waathirika wakubwa
ni wananchi wasio na hatia hasa wanawake na watoto
Matembezi
hayo ya siku ya kimataifa ya matembezi ya amani na kupinga dhulma wanayofanyiwa
wapalestina ambayo yamebeba kauli mbiu “TUWAONEE HURUMA WAPALESTINA”
No comments