Breaking News

SERIKALI YAMILIKI HISA ZA TTCL KWA ASILIMIA 100

By Frank on June 23, 2016
C1Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel Afrika Bwana Christian Manuel De Faria (aliye kaa katikati)  na Bwana Lawrence Mafuru, Msajili wa Hazina ( aliye kaa wa kwanza kushoto) wakiweka saini ya kuiwezesha Serikali kumiliki hisa za TTCL kwa asilimia 100.  Dkt. Injinia Maria Sasabo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (aliyesimama nyuma katikati), Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL (aliyesimama wa tatu kushoto) na Dkt. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL (aliyesimama wa pili kushoto) wakishuhudia tukio hilo.
C2 
Msajili wa Hazina Bwana Lawrence Mafuru akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utiaji saini na Bharti Airtel kwa niaba ya Serikali ili iweze kumiliki hisa 100 za TTCL
C3 
Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) Dkt. Injinia Maria Sasabo akiishukuru kampuni ya Bharti Airtel ya kuuza hisa 35 ili Serikali iweze kuendeleza mikakati yake ya kuimarisha TTCL. Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL (wa kwanza kulia) na Bwana Lawrence Mafuru, Msajili wa Hazina (wa kwanza kushoto) wakifuatilia tukio hilo.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imefanya makabidhiano ya hati ya kuiwezesha Serikali Kumiliki Hisa za Kampuni ya TTCL kwa asilimia 100 ambapo hisa ailimia 35 zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Bharti Airtel.
Utiaji saini huo umefanyika baina ya Bwana Larewnce Mafuru, Msajili wa Hazina na Bwana Christian Manuel De Faria, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Afrika.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2016 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kushuhudiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Dkt. Injinia Maria Sasabo, Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL na Dkt. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Kabla ya tukio hilo la leo, Serikali kupitia TTCL ilikuwa ina miliki hisa hizo kwa alisimia 65 na Bharti Airtel kwa asilimia 35.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

No comments