Breaking News

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015 KUTOKA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

R7 
Rais wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli akitoa hutuba yake mbele ya viongozi mbali mbali na mabalozi wa nchi za nje baada ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo
R4 
Rais wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) kutoka kwa Jaji Mstaafu wa Tume hiyo Mhe,Damian Lubuva mbele ya Viongozi mbali mbali na mabalozi wa nchi za nje  katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo,[Picha na Ikulu.] 23/06/2016.
R5 
Rais wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mhe,Dkt.John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe,Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakionesha Ripoti ya Tume hiyo Juu baada ya kukabidhiwa rasmi leo katika ukumbi wa mikutano Ikulu ya Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.] 23/06/2016.
R6  
Baadhi ya Mawaziri na Viongozi wengine wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli alipokuwa akitoa hutuba yake mbele ya viongozi hao na waalikwa wakiwepo mabalozi wa nchi za nje baada ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leoR8 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi (kushoto) Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Nne Mhe,Jakaya Mrisho Kikwete(katikati)na Waziri Mkuu mstaafu Mhe,Ahmed Salum(kulia) wakiwa katika hafla ya kukabidhi Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo,
R9 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya kukabidhi Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo,
R2 
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa katika hafla ya kukabidhi Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania (NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo
R1 
 Makamo wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Mhe,Philip Mangula akiwa na Mabalozi mbali mbali wa Nchi za Nje wakiwa   katika hafla ya kukabidhi Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania (NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leoR10 
Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) na Waalikwa mbali mbali wakiwa katika hafla ya kukabidhi ripoti ya Tume hiyo ya Uchaguzi  kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt.John Pombe Magufuli  katika ukumbi wa mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo,
[Picha na Ikulu.]

No comments