HII NDIO KAULI YA WAZIRI MKUU MHE, KASSIMU MAJALIWA KWA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA.
Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa
ameagiza wakuu wa wilaya na mikoa kufanya ziara katika maeneo yao hasa
vijijini ili kujua matatizo ya wananchi wao kwa ukaribu na kuyapatia
ufumbuzi.
Mhe.Majaliwa ameyasema hayo leo
hii Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wakuu wa wilaya na mikoa
walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda
kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa
wakuu wa mikoa na wilaya waache kukaa maofisini mwao badala yake
watembelee wananchi na hasa wale wa hali ya chini ili kujua matatizo yao
ya Ardhi na kupatia ufumbuzi migogoro ya wafugaji na wakulima.
Pia Mhe.Majaliwa amewasisitiza
wakuu hao kutambua kwamba majukumu waliyonayo ni makubwa na wananchi
wana mategemeo makubwa juu yao na hivyo ni budi wakatekeleza wajibu wao
na kuhakikisha watanzania wanapata huduma zote za muhimu kwa kutumia
elimu, uwezo, uadilifu, uaminifu na uwajibikaji walionao ili kufanikisha
maendeleo kwa wananchi.
Aliongeza kuwa wakuu hao wana
jukumu kubwa la kusimamia pesa za serikali pesa za miradi zinakokwenda
katika halmashauri za wilaya zao na kukazia kuwa Serikali haitasita
kuchukua hatua kwa yeyote ambaye hatofanya kazi zake kikamilifu.
Waziri mkuu amewaagiza wakuu wa
Mikoa kushirikiana kwa karibu na wakuu wa Wilaya ili kutafuta ufumbuzi
wa matatizo ya maeneo yao kwani wananchi wana kiu ya maendeleo katika
maeneo yao.
Na Daudi Manongi, MAELEZO
No comments