DIWANI KATA YA MABIBO ASIFU VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA,MABUNGE YA JAMII, ATOA RAI KWA WENZAKE KUWAPA USHIRIKIANO
Diwani wa kata
ya Mabibo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dare Salaam Kassim Lema amesifu
ushirikiano ambao umeanza kujitokeza kutokana na uwepo wa mabunge ya jamii na
vituo vya taarifa na maarifa katika kata yake na kusema kazi wanayoifanya ni
kubwa wanastahili kuungwa mkono kwa msaada wowote wanaoutaka.
Akizungumza katika
mjadala kati ya viongozi na wanajamii huko Tgnp Mtandao, Lema amesma uwepo wa
wa vituo vya taarifa na maarifa vinasaidia kuibua kero za wananchi na kueneza
elimu kwa umma kuhusu miradi mbalimbali ndani ya kata.
Ameongeza
kusema, uwepo wa vituo hivyo vya taarifa na maarifa pamoja na mabunge ya jamii
kumechochea uwazi na uwajibikaji hivyo angeomba viongozi wengine kutoa
ushirikiano kwa vituo hivyo ikiwamo kutoa takwimu mbalimbali wanazotaka.
“Niseme ofisi
yangu kama diwani iko wazi muda wowote, nimegundua vituo hivi si maadui badala
yake vinasaidia kuibua kero za wananchi tunaowahudumia. Kata ni yetu sote hivyo
kupanga pamoja ni jambo la faraja” Alisema Kassim Lema.
Aidha awali
akifungua mjada huo uliowakutanisha vituo vya taarifa na maarifa kutoka kata ya
tatu za Makumbusho, Mabibo na Kipunguni, Kaimu Mkurugenzi wa Tgnp Mtandao
Gloria Sechambo amesema mjadala huo umelenga kuangalia utekelezaji wa mradi na
ufanisi wake toka umeanza kufanya kazi miezi mitatu iliyopita
“Leo Tumewakutanisha kwa pamoja jamii,
viongozi na wanaharakati katika mjadala huu ili kubalishana uzoefu juu ya
utekelezaji wa mradi, kama mnavyoona wananchi wanasema mradi umeanza kuonyesha
matokeo yake ikiwamo kutokomeza ngoma za vigodoro katika kata hizo”Alisema
Gloria Sechambo.
Kwa upande wake
Bw Selemani Bishagaazi, mwenyekiti wa Bunge la jamii kata ya Kipunguni amesema
sasa viongozi wameanza kuelewa kuwa si kila kitu wanaharakati wamekuwa
wapingaji badala yake ni sehemu ya msaada wa kufanya maendeleo ya kata kusonga
mbele.
Amesema ilikuwa
ngumu kwa viongozi wa kata kuelewa wao wanafanya nini, lakini sasa wamekuwa
wanapata ushirikiano katika mabunge yao na hiyo inawasaidia kuweza kuishauri
serikali ya kata katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, mapambano
katika kuleta maendeleo hususani sekta ya maji safi na salama,elimu na afya
No comments