TRA YAKUTANISHA WADAU WA KODI KUJADILI UANZISHWAJI WA CHOMBO CHA KURATIBU NA KUSIMAMIA WANATAALUMA WA KODI
Katika kuendelea kuimarisha
ushirikiano uliopo kati ya walipa kodi na wakusanyaji wa kodi, Mamlaka
ya Mapato nchini (TRA) imefanya kongamano la pamoja na wadau wa kodi
nchini likiwa na lengo la kujadili kwa pamoja kuhusu uanzishwaji wa
chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi
wa kongamano hilo, Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na
Mipango, Shogholo Msangi alisema wamekutanisha wadau hao wa kodi ili
waweze kutoa maoni na kukubaliana kwa pamoja jinsi gani chombo hicho
kitaweza kufanya kazi.
“Kutakuwa na chombo ambacho
kitakuwa kinaratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi na lengo ni kupitia
kongamano hilo wadau wa kodi wataweza kukubaliana kwa pamoja kuona ni
jinsi gani chombo hicho kitafanya kazi,
Kamishna wa Sera na Bajeti
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi akitoa neno la
ufunguzi katika kongamano lililoandaliwa na TRA na kukutanisha wadau
mbalimbali wa kodi. (Picha zote na Rabi Hume – MO Blog)
“Unaweza kukuta kuwa mlipa kodi
kwa sasa ndiyo anaumia au TRA ndiyo inaumia lakini chombo hicho
kitaweza kusimamia na kuweka kila jambo sehemu sahihi kama linavyotakiwa
kuwapo,” alisema Msangi.
Nae Mkuu wa Chuo cha Taifa cha
Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo alisema kuwa chombo hicho kama
kikianzishwa kitaweza kufanya kazi zake kwa uhuru bila kuingiliwa na TRA
ili kuhakikisha kuwa kinatoa na haki kati ya mlipa kodi na wakusanyaji
wa kodi (TRA) bila kuumiza upande wowote kwani jambo hilo linawahusu
wote.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Kodi
(ITA), Prof. Isaya Jairo akitoa neno la ukaribisho katika ufunguzi wa
kongamano hilo lililofanyika Bagamoyo, Pwani.
Alisema kupitia kongamano hilo
wamekutanisha wataalam wa kodi, wahasibu, walipa kodi, wanasheria,
washauri wa kodi na walimu wa kodi kutoka vyuoni ili kuweza kupata maoni
ya pamoja na kupata maoni ya makubaliano ya pande zote ambayo
yatatumika katika kuendesha chombo hicho.
Baadhi ya wadau waliohudhuria kongamano hilo la siku moja lililofanyika Bagamoyo, Pwani.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja
Picha – MO Blog
No comments