Breaking News

CUF YATOA USHAURI HUU KUELEKEA BUNGE LA BAJETI, WASISITIZA KUWEPO NA UWAZI UTEKEREZAJI WAKE

Dar es salaam- Chama cha wananchi (CUF) kimeitaka serikali kuwatendea haki Watanzania kwa kutoa ufafanuzi kwa nini Malengo ya Mpango wa tatu wa Maendeleo ya Taifa hayajafikiwa licha ya kuwepo mikakati mingi ya utekelezaji.

Akizungumza makao makuu ya chama hicho buguruni mapema leo Aprili 6, 2025 wakati akitoa mtazamo kuhusu bajeti ya Mwisho ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo 2021/22 hadi 2025/26 amesema hotuba za Mawaziri wa sekta nazo ziikite katika kuwaeleza Watanzania sababu za kushindwa kwa serikali kutekeleza Mpango wa Tatu wa Maendeleo katika sekta zao.

"Nitoe rai kwa Serikali kuwa na kwa kutambua umuhimu wa watanzania itoe Mawaziri mkuu hotuba na mawaziri wa sekta nazo ziikite katika kuwaeleza Watanzania sababu za kushindwa kwa serikali kutekeleza Mpango wa Tatu wa Maendeleo katika sekta zao". Alisema Prof. Lipumba.

Alisema hotuba hizo zichambue sababu za kutofanikisha malengo ya Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo hili watanzania watambue sababu za kushindwa kwa serikali kutekeleza Mpango wa Tatu wa Maendeleo katika sekta zao.

Aidha Prof lipumba aliongeza kuwa kwa Utaratibu uliozoeleka hotuba za Bunge la Bajeti uanza na hotuba za Waziri wa Mipango na Waziri wa Fedha kwa kueleza hali ya uchumi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo na mapendekezo ya mapato na matumizi. 

Amesema kwa kinachoendelea sasa hotuba hizi ni za mwisho katika Bunge la bajeti, kwani anayefungua dimba ni Waziri Mkuu ambaye anaeleza utekelezaji wa mipango ya serikali kwa ujumla, hivyo ni vema akaanza kuwaeleza wananchi kwa nini Serikali imeshindwa kutekeleza Mpango huo. 

"Kwa mujibu wa ratiba ya bunge kikao cha Bunge la Bajeti kinatarajiwa kuanza Aprili 8, 2025 hii ni bajeti ya mwisho ya utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo 2021/22 – 2025/26 na mwaka wa mwisho wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025" Alisema Prof. Lipumba.

Alisema Machi 11, 2025, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, aliwasilisha Bungeni mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2025/26. Pia Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, naye aliwasilisha Bungeni, Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 ambapo Serikali inapanga kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 57.04 kwa mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 ya shilingi trilioni 50.29.

Katika hatua nyingine Prof. Lipumba akizungumzia ukuaji wa uchumi amesema Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, alieleza kuwa ukuaji wa uchumi umefikia asilimia 6 mwaka 2025 kutoka asilimi 5.4 mwaka 2024 Mfumko wa bei kuwa kati ya asilimia 3.0 – 5.0.

Kwamba mapato ya ndani kufikia asilimia 16.4 ya Pato la Taifa mwaka 2025/26 ukilinganisha na matarajio ya asilimia 15.8 mwaka 2024/25 ambapo mapato ya kodi kufikia asilimia 13.1 ya Pato la Taifa mwaka 2025/26 ukilinganisha na matarajio ya asilimia 12.8 mwaka 2024/25.

Alisema kwa mujibu wa taarifa hiyo inaonyesha kuwa Serikali inatarajia kukusanya shilingi trilioni 40.97 kutoka vyanzo vya ndani, sawa na asilimia 69.7 ya bajeti yote ambapo Shilingi trilioni 16.07, sawa na asilimia 30.3 ya bajeti inatarajiwa kupatikana kupitia mikopo ya ndani na nje.