Breaking News

SHILOLE ATANGAZWA KUWA BALOZI WA MAFUTA YA KUPIKIA YA KORIE

Dar es salaam - Msanii na mfanyabiashara mashuhuri nchini Tanzania, Bi. Zuwena Mohammed maarufu kama (Shilole) ametangazwa rasmi kuwa balozi wa Mafuta ya Kupikia ya Korie akiongeza mvuto wake mkubwa kwa chapa hiyo iliyoboreshwa kwa mwonekano mpya na vifungashio vipya.

Bi Shilole ambae aliongoza uzinduzi wa vifungashio vya nusu lita na robo lita vya mafuta ya Korie, amesema hatua hiyo imelenga kuwafanya Watanzania wengi zaidi kupata mafuta ya kupikia yenye ubora kwa urahisi na kwa bei nafuu.

Akizungumza wakati wa hafla ga uzinduzi huo, Shilole amesema leo ni siku muhimu sana kwa kushiriki tukio hili kubwa na "Korie Kipochi" imefika kwa mikono sahihi na kwa wakati sahihi! Hata unapomaliza mafuta ghafla, Korie Kipochi ni suluhisho la haraka kwa dharura za jikoni.

"Vifungashio vipya vimetengenezwa kwa mifuko laini ya plastiki chini ya jina "Kipochi" yanapatikana madukani kote nchi nzima kwa bei nafuu na lengo kubwa ni kuwafikia walaji wa kipato cha chini". Alisema Bi Shilole

Alisema Lengo kuja na ubunifu huo ni kusaidia familia hususani za kipato cha chini kuweza kupunguza gharama za chakula bila kuathiri ubora wa bidhaa wanazotumia.

Aidha aliongeza kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20 mafuta ya Korie yamekuwa sehemu ya familia nyingi nchini Tanzania na hatua hii mpya inathibitisha dhamira yake ya kuwafikia watumiaji wote.

kwa upande wake Meneja na Mauzo wa Murzah Wilmar ambao ndio watengenezaji na wasambazaji wa mafuta ya Korie nchini, Bw. Steven Ford alisisitiza kuwa kampuni hiyo inajali afya za walaji wake, "Lengo letu ni kuhakikisha Watanzania wote wanapata mafuta bora na salama kwa bei nafuu, hasa wale wanaohitaji chaguo rafiki kwa mfuko wao."

Aliongeza kuwa ni muhimu kwa walaji kununua bidhaa zilizoidhinishwa na TBS na kuuolea mfano tukio lililotokea Yombo Dovya, ambapo mafuta yasiyo salama yalileta madhara makubwa kwa afya za watu.

"Nitoa wito Kwa wanachi wote nchini kutumia mafuta yaliyoidhinishwa, mnalinda afya zenu na kuepuka na kujilinda na madhara mbalimbali yanayoeeza kutoea kwa kutumia bidhaa bandia". Alisema Bw. Ford 

Alisema ingawa masharti ya Mkataba wa ushirikiano wa Shilole na Murzah Wilmar yamebaki kuwa siri, jambo moja ambalo liko wazi kupitia ushawishi wake utaisaidia Korie Kipochi kufika katika kila kona Tanzania na kuhakikisha kila familia inapika kwa mafuta salama na yenye ubora wa hali ya juu. 

No comments