Breaking News

MKUTANO WA 19 JUKWAA LA KOROSHO AFRIKA 2025 KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

Na NeemaMpaka, Dar es salaam - Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Jukwaa la Korosho Afrika 2025 unakusudia kutangaza fursa za uwekezaji zilizoko kwenye Tasnia ya Korosho kuanzia shambani.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo Januari 31, 2025  jijini dare es salaam  wakati wa uzunduzi wa mkutano huo unaotarajiwa kufanyika  November 18 Hadi 22 jijini dare es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Francis Alfred amesema.

"Tunategemea kupata uwekezaji kwenye mashamba makubwa ya korosho, kuongeza ubanguaji ambapo matarajio ni kuongezeka kwa viwanda vya kubangua na kusindika korosho na bidhaa zake na kuimarika kwa masoko kwa kufungua masoko ya korosho na bidhaa zake ndani na nje ya nchi za Afrika," amesema Alfred na kuongeza,

"Naomba kuwashukuru African Cashew Alliance (ACA) kwa maamuzi yake ya kuridhia Mkutano wa 19 wa mwaka 2025 kufanyika nchini Tanzania ikiwa ni mara ya tatu ambapo mara ya kwanza ulifanyika mwaka 2007 na mara ya pili 2019. Mkutano huu hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka 2024 ulifanyika nchini Benin,".

Kuhusu wazo kuu na kauli mbiu ya mkutano huo Alfred amebainisha kuwa wazo kuu ni "kufungua fursa za uwekezaji kwenye tasnia ya Korosho Kwa ukuwaji wa uchumi endelevu (Unlocking Cashew Investment Opportunities for Sustainable Economic Growth) huku  kauli mbiu ikiwa  ni "Wekeza kwenye Korosho kwa Maendeleo endelevu (Invest in cashew for Sustainable Development). 

Wazo kuu na kauli mbiu vinaendana na malengo ya Mheshimiwa Dk Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayokusudia kuuza korosho zilizoongezwa thamani badala ya kuendelea kuuza korosho ghafi. 

Kwamba Mkutano huo utatumika kuhamasisha matumizi ya korosho na bidhaa zake kama vile mafuta ya ganda la korosho (Cashewnut Shell Liquid - CNSL), sharubati (juice), maziwa ya korosho (cashew milk), mvinyo (wine), nyama ya mabibo (cashew apple meat) na pombe kali.

Alfred ameeleza bidhaa nyingine kama ethanol zinaweza kutumika kwenye maabara za hospitali na shule zetu na hivyo kupanua wigo wa soko la korosho. 

Akizungumzia kuhusu juhudi za Serikali kuendeleza zao hilo alifafanua kuwa Serikali ya Awamu ya sita imefanya juhudi kubwa za kuendeleza zao la korosho ambapo kwa kipindi cha miaka mitatu sasa imekuwa ikitoa pembejeo za korosho kwa wakulima kwa ruzuku ya asilimia 100.

Ametoa mfano katika msimu wa 2024/2025 ambapo ruzuku ya pembejeo ilikuwa shilingi billioni 182 ambapo utoaji wa pembejeo za ruzuku umechagiza kuongezeka kwa uzalishaji kutoka tani 310,000 msimu wa 2023/2024 hadi kufikia tani 410,000 kwa msimu wa 2024/2025 zilizouzwa kupitia minada. 

Amesema ukusanyaji wa taarifa za uzalishaji unaendelea kwa kukusanya takwimu za korosho zinazobanguliwa majumbani kwenye vikundi vidogo na watu binafsi pamoja na uzalishaji katika mikoa mipya. 

Kwamba hadi  mwisho wa msimu makadirio ni kuzalisha jumla ya tani 500,000 katika msimu wa 2024/2025. Ameongeza Aidha bei ya korosho ghafi katika msimu wa 2024/2025 iliimarika na kufikia shilingi 4,195 kwa kilo ikiwa ni bei ya juu kuliko bei zote zilizopatikana kutoka nchi yetu ipate uhuru. 

Ameeleza, pamoja na uwepo wa mahitaji makubwa ya korosho ghafi katika soko la dunia, Uamuzi wa Serikali kutumia mfumo wa mauzo wa Soko la Bidhaa (TMX) umesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ushindani katika minada na kuchangia katika kuimarika kwa bei.Pamoja na mafanikio hayo lengo la Serikali ni kuzalisha tani 1,000,000 za korosho ghafi ifikapo mwaka 2029/2030. 

Alfred amesema katika juhudi za kufikia malengo hayo Wizara ya Kilimo kupitia Bodi ya Korosho imeajiri Vijana 500 kupitia mpango wa jenga kesho iliyo bora (Building a Better Tomorrow) ambao wana jukumu la kusaidia katika utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima pamoja na kusimamia shughuli mbalimbali za uendelezaji wa zao katika kata zote zinazolima korosho katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga. 

Ameeleza kuwa Vijana hao watapewa pikipiki pamoja na vishikwambi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Aidha, katika kufikia lengo la kubangua korosho zote zinazozalishwa hapa nchini

No comments