BATA LA "NISHATI SAFI" KUFANYIKA FEBRUARI 8 JIJINI DAR
Mratibu wa tamasha la Bata la Nishati safi Bw. Steven Nchimbi akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi ya tamasha Bata la Nishati safi litakalofanyika Feb 8, 2025 jijini dar es salaam.
Afisa Mazingira wa Manispaa ya Kinondoni, Bi.Hawa Shaban akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea tamasha la Bata la Nishati safi litakalofanyika Feb 8, 2025 jijini dar es salaam.
Mwakilishi wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia, Patcho Mwamba akizungumzia namna bendi hiyo ilivyojipanga kutoa burudani siku ya tamasha la Bata la Nishati safi litakalofanyika Feb 8, 2025 jijini dar es salaam.
Dar es salaam - Jukwaa la Waandishi wa habari Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Manispaa ya Kinondoni limeandaa tamasha kubwa lijulikanalo "Bata la Nishati" litakalofanyika Februari 8, 2025 katika eneo la Mbweni Round about ya Ndege Beach Uwanja wa Mpira Jijini Dar es salaam ikiwa lengo ni kuhamasisha matumizi ya Nishati safi na salama.
Kwa mujibu wa Taarifa imetolewa leo Februari 1, 2025 na Mratibu wa tamasha hilo Bw. Steven Nchimbi wakati akizungumza na Waandishi wa habari, nakubainisha kuwa tamasha hilo litakua la aina yake huku likitarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Wananchi.
Aidha Nchimbi amesema kwamba tamasha hilo limeandaliwa kwa lengo la kuunga mkono ajenda ya Serikali ya Matumizi ya Nishati safi nakuachana na Matumizi ya Nishati chafu inayosababisha athari za kiafya pamoja na Mazingira.
"Atakae hitaji kujumuika nasi kwenye tamasha hili atachangia kiasi cha shilingi elfu thelathini na tano tuu (35,000) hii pesa itamsaidia kupata t-shirt pamoja na kofia ambazo atazitumia kwenye eneo la tukio" alisema Nchimbi nakuongeza
"kutakuwepo na mbio za Marathon kilometa mbili na nusu, pamoja na kilometa tano,halafu pia kutakuwepo na zoezi la upimaji wa afya bure, burudani ya muziki mubashala kutoka bendi ya kundi la FM Academia linalo ongozwa na Patcho Mwamba, pamoja na kuchoma nyama bure kwa kutumia Nishati safi, hivyo wananchi naomba wajitokeze kwa wingi."
Nchimbi amefafanua kuwa kwa mtu atakaehitaji kuchangia fedha kwa ajili ya kushiriki tamasha hilo anapaswa kutumia namba ya kulipia ambayo ni 16154388 jina ni M.B.I ONLINE TV au kupitia benki ya CRDB namba 0133914590500 jina ni EAST AFRICA JOURNALIST FORUM.
Amesema kuwa umefika wakati wa watu kuachana na matumizi ya Nishati chafu na kutumia Nishati safi ili kuendana na malengo ya Dunia ya kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi yatokanayo na hali ya kutohifadhi Mazingira.
Kwa upande wake Afisa Mazingira wa Manispaa ya Kinondoni, Bi.Hawa Shaban amesema kuwa tamasha hilo litasaidia kutoa Elimu kwa jamii wilayani humo pamoja na maeneo mengine kuhusu matumizi ya Nishati safi ya kupikia pamoja na kutoa fursa za kiuchumi.
Amesema kuwa Wilaya hiyo inaendelea kutoa Elimu kwa jamii kuhakikisha inaondokana na dhana ya matumizi ya Nishati chafu ya kupikia kama vile kuni,nakuweza kutumia Nishati safi kama vile gesi ya kupikia,mkaa mbadala,pamoja na gesi itokanayo na takataka zinazozalishwa kwenye jamii.
"Tamasha hili linaunga mkono agenda ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha asilimia zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia Nishati safi ifikapo mwaka 2035,na kuanzia leo Februari mosi 2025 taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya mia moja kama vile Shule,Vyuo,taasisi za ulinzi na usalama,zinatakiwa kufikia kikomo kutumia Nishati chafu nabadala yake zianze kutumia Nishati safi" amesema Afisa Mazingira huyo.
Nakuongeza kuwa,tamasha hilo pia limelenga kutoa Elimu kwa jamii kuhusu kuchangamkia fursa ya kutengeneza mkaa mbadala ambao unatokana na takataka hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kushiriki katika tamasha hilo.
Nae Meneja Masoko wa Kampuni ya Mfugale Ferniture.BiLoyce Cornery amesema kwamba kampuni hiyo imeungana na waandaji wa tamasha hilo kuweza kutoa Elimu juu ya Matumizi ya Nishati safi,ili kuondokana na tabia ya kukata miti hovyo kwasababu inasababisha uharibifu mkubwa wa Mazingira.
Akizungumzia tamasha hilo Kiongozi wa bendi ya muziki wa dansi kutoka kundi la FM Academia Patcho Mwamba amesema kwamba bendi hiyo itatoa burudani ya kukonga nyoyo za mashabiki na wapenzi wa burudani ya muziki wa dansi,huku akiwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushirikia katika tamasha hilo.
No comments