Breaking News

DOROTHY SEMU: TUKO TAYALI KUTASHIRIKIANA NA VYAMA MAKINI UCHAGUZI MKUU 2025

Dar es salaam - Kiongozi wa Chama Chama Cha ACT Wazalendo amesema Dorothy Semu amesema chama kipo tayali kitaunganisha nguvu na vyama vyote makini sambamba na wadau wa demokrasia nchini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa lengo la kuiondoka madarakani CCM.

Akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu Makao Makuu ya Chama hicho Magomeni jijini Dar es Salaam, Bi Semu amesema chama kipo tayali kuunganisha nguvu na vyama vingine makini pamoja na wadau wa demokrasia nchini kuhakikisha kuwa wanaing'oa CCM madarakani

"Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ni muhimu na tunatambua kwamba kuna hujuma na hila zinazotumiwa ili kukatisha tamaa wananchi. Hali hii inatufanya tuwe na jukumu kubwa la kusukuma ajenda ya kuunda jukwaa la mapambano ya pamoja na vyama makini,". Alisema Bi. Semu 
Alisema kupitia ushirikiano huo tunahitaji kufanya shughuli za pamoja ili kuimarisha umoja wetu wenye nguvu utakao leta tija ya mabadiliko. Tunahitaji kupambania kuurejesha uchaguzi. Nchi yetu hasa hakuna uchaguzi, tuna uchafuzi.

Bi Semu aliongeza kuwa viongozi, wanachama na wananchi wanaendelea kupoteza matumaini kutokana na mwenendo usioridhisha wa chaguzi nchini ambapo umekuwa ukiipendelea CCM.

Kwa kutambua hili Chama kimejipanga vizuri kuhakikisha kuwa kinadhibiti hujuma zote za CCM na dola katika kunafanikisha malengo yake ya kisiasa kama ambavyo majemedari hodari kwenye vita mbalimbali ulimwenguni waliweza kuusoma mwelekeo wa vita, kufufua ari ya mapambano na kusonga mbele hadi kuupata ushindi.
"Ni vizuri kukumbushana kuwa pamoja na hayo yote uchaguzi ni kama Vita. Vita ina majira yake. Kuna wakati wa faraja ya ushindi na kuna wakati wa majanga katika vita (casualities). Kuna wakati wa ari ya kimapambano kutokana na dalili ya ushindi au ushindi kwenye baadhi ya mapambano na kuna kipindi cha kuvunjika ari kutokana na kupoteza baadhi ya mapambano (battles),". Alisema Bi Semu

Alisema Wajibu wa jemedari mzuri ni kutambua hali halisi katika vita na kuchukua hatua stahiki. Jemedari hapaswi kukata tamaa, bali anapaswa kuchukua hatua stahiki kulingana na hali halisi. Chama chetu kipo katika hali ya vita inayotokana na mazingira yanayokatisha tamaa.
Kwa mshikamano wetu, hakika tutayafikia malengo yetu. Ndugu zangu, ni wakati wa kuchukua hatua. Tuwe na mshikamano na umoja katika kukabiliana na matatizo yanayotukabili. Kwa pamoja, tunaweza kufanikisha malengo yetu na kuleta mabadiliko tunayoyahitaji,"

Aliendelea kusema "Wajibu wetu kama majemedari katika vita yetu ni kuhakikisha kuwa hatukati tamaa. Iwapo Wajumbe wa Halmashauri Kuu tutakata tamaa, hilo litakuwa ni tamko la kushindwa vita, jambo ambalo hatuwezi kuliruhusu kutokea,"





No comments