WAZIRI DKT. CHANA AKABIDHI VITENDEA KAZI KWA TFS
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana akikata utepe kuzindua vitendea kazi vya TFS vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6, vikiwemo matrekta, Motor Grader, na malori 6. Uzinduzi umefanyika Jengo la Mpingo, Dar es Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana akifafanua jambo wakati akizungumza katika hafla ya Kukabidhi vitendea kazi kwa TFS vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6, vikiwemo matrekta, Motor Grader, na malori 6. Uzinduzi umefanyika Jengo la Mpingo, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Brigedia Jenerali, Mbaraka Mkeremy akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa vitendea kazi vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6, vikiwemo matrekta, Motor Grader, na malori 6. Uzinduzi umefanyika Jengo la Mpingo, Dar es Salaam.
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Prof. Dos Santos Silayo akizungumza katika hafla kukabidhiwa vitendea kazi vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6, vikiwemo matrekta, Motor Grader, na malori 6. Uzinduzi umefanyika Jengo la Mpingo, Dar es Salaam
Dar es salaam - Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amekabidhi magari na mitambo Kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) vitendea kazi vya TFS vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6, vikiwemo matrekta, Motor Grader, na malori 6. Uzinduzi umefanyika Jengo la Mpingo, Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Dkt. Chana amesema ni matumaini yake kuwa vifaa atanavyokabidhi leo pamoja na vile vingine ambavyo vilishapokelewa vitakwenda kwenye kazi zilizokusudiwa.
Ametaja malengo hayo kuwa, kwanza, vitatumika kwa malengo na kazi zilizokusudiwa ambazo ni kuimarisha miundombinu ya barabara katika mashamba ya miti, doria na usimamizi wa rasilimali misitu na nyuki kwa jumla.
"Pili, vitatunzwa ili viweze kutoa huduma bora kwa muda mrefu, Tatu, kwa kupata vyombo hivi tutaona mabadiliko ya usimamizi wa misitu, rasilimali nyuki na usimamizi wa mashamba ya miti nchini," alisema Waziri Chana na kuongeza,
"Nne, kupatikana kwa vyombo hivi kutaimarisha utekelezaji wa shughuli za Jeshi la Uhifadhi kwa ujumla. Maafisa na Askari, Naomba nimalizie hotuba yangu kwa kuwaasa TFS kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza sasa,".
Waziri Chana alisema kuna fursa mbalimbali za uwekezaji katika biashara ya kaboni katika misitu yenu, uwekezaji wa miundombinu ya malazi, kuanzisha shughuli mpya za utalii kwenye misitu ya hifadhi ya mazingira asilia, mashamba ya miti na mikoko.
"Changamkieni fursa za kimataifa kwa kuendelea kuandaa maandiko ya kimkakati kupata fedha za miradi ya maendeleo ili kuongeza rasilimali za usimamizi wa misitu yetu," alisema Waziri Dkt. Chana.
Katika hatua nyingine Waziri Chama ameipongeza Menejimenti ya Wakala kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa kununua vitendea kazi kila mwaka, ujenzi wa majengo ya ofisi na nyumba za watumishi.
"Nimejulishwa kuwa mmepiga hatua kubwa sana katika ujenzi wa nyumba na majengo ya ofisi na vituo vya ulinzi (Ranger posts) ambapo katika miaka hii mitatu mmefanikiwa kujenga majengo mapya zaidi ya 60 na kununua magari na mitambo zaidi ya 72,". alieleza Waziri Chana.
Alisema hali hii inaongeza motisha ya kazi na kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa Majukumu yao.
Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Prof. Dos Santos Silayo alisema vifaa vilivyopokelewa na kuzinduliwa ni vitendea kazi yakiwemo matrekta matatu (3) na tela zake, Motor Grader moja (1); na Malori 6 ambayo yanajumuisha (Lori (box body) tatu (3), Lori (tipa) tatu (3) yenye thamani ya Shilingi 2,674,923,059.
Alisema vifaa hivyo ni kwa ajili ya kwenda kutumika kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya usimamizi wa rasilimali adimu za misitu na nyuki.
No comments