Breaking News

DKT. SAMIA MGENI RASMI TUZO ZA ULIPAJI WA KODI

Dar es salaam - Rais Dokta Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni katika tuzo ya walipaji kodi wazuri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwaka 2023/24 ambayo inatarajiwa kufanyika Januari 23 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Elimu na Mawasiliano TRA, Richard Kayombo amesema hayo jana nakuongeza kuwa mfanyabiadhara atayefanikiwa kunyakuwa tuzo hiyo ni yule akiyekithi vigezo ikiwa ni pamoja na walipa kodi waliofuta sheria za kodi na kulipa kwa wakati na hiari,walipa kodi waliolipa kiasi cha kodi kikubwa kwenye ngazi ya wilaya, mkoa na taifa,utunzaji wa nyaraka za sahihi za forodha.

Kayombo alisema tuzo hizo ni muendelezo wa tuzo za TRA zinazotolewa kila mwaka na sasa ni mwala wa 15 tuzo hizo zinafanyika hapa nchini na niheshima kwa wafanyabiashara waliokuwa katika makundi manne ikiwemo wilaya, mkoa, taifa na kisekta kupewa tuzo hizo na Rais kwani watatambulika na Kiongozi Mkuu wa Nchi kuwa ni mongoni wa wafanyabiashara wanaochangia maendeleo ya nchini na Taifa kwa ujumla.

Alisema wafanyabiashara waliolipa kodi kwa shuruti hawatakuwa na sifa za kuingia katika tuzo hiyo kwani hawakufanya hivyo kwa hiari na tuzo hiyo itakuwa na Majaji makini wenye vigezo vilivyotukuka katika kuwachambua washindi watakaukuwa na sifa stahiki.

Mkurugenzi huyo alisema lengo la tuzo ni kutambua umuhimu wa mlipa kodi kwa kulipa kodi bila kusukumwa na kujua wajibu wake katika kufanya biashara na kuzingatia kulipa kodi lwa maendeleo ya nchi.

“Sifa za tuzo ni pamoja nankulipa kwa hiari ,kuzingatia kutumia mashine ya kulipa kodi ya EFD, kutohusika na ukwepaji kodi na kuboresha ulipaji kodi mwaka hadi mwaka” alisema Kayombo.

Alisema mwaka huu jumla ya walipa kodi na wadau 1228 watatunukiwa vikombe,ngao na vyeti ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao katika kujenga Taifa kupitia ulipaji wa kodi kwa hiari au kwa kusaidia TRA kwa njia moja au nyingine katika ukusanyaji wa mapato.

No comments