TAWA ZINGATIENI SHERIA ZA UWEKEZAJI WA UWINDAJI WA KITALII - WAZIRI CHANA
Dodoma - Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ameitaka menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya Serikali katika uwekezaji kwenye vitalu vya uwindaji kwa maslahi mapana ya Taifa.
Ameyasema hayo leo Januari 18, 2025 katika kikao kilichofanyika ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma.
“Hakikisheni maeneo yenye vitalu vya uwindaji wa kitalii yanakuwa salama yasivamiwe na mifugo ili wawekezaji waweze kuona thamani ya uwekezaji wao na pia ili kuongeza idadi ya wageni wanaokuja kuwinda” amesisitiza Mhe. Chana.
Kikao hicho kiliambatana na kupitia taarifa mbalimbali za uwekezaji kwenye maeneo ya uwindaji wa kitalii.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Kaimu Kamishna Uhifadhi TAWA, Bw. Mlage Kabange, Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Fortunata Msoffe na baadhi ya watumishi waandamizi kutoka TAWA.
No comments