Breaking News

AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAWAZAWADIA WASHINDI WA KAMPENI YA TWENDE KIDIGITAL TUKUVUSHE JANUARI

Na Mwandishi wetu - Dar es salaam - Akiba Commercial Bank imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni "twende kidigital tukuvushe Januari" na imewahimiza kuendelea kutumia huduma zake za kidijitali kama vile ACB Mobile, Internet Banking, ACB VISA Card, na ACB Wakala ili kufurahia uzoefu wa kipekee wa kibenki.

Shukrani hizo zimetolewa Jijini Dar es salaam Januari,2025 Mkuu wa Kitendo cha biashara Akiba Commercial Bank Plc Dkt. Danford Muyango Akiba wakati wa hafla ya kuwazawadia Washindi wa Kampeni ya droo ya kwanza ya kampeni ya "Twende Kidijitali, Tukuvushe Januari," ambapo wateja kadhaa kutoka Dar es Salaam na mikoani walipokea zawadi za fedha zilizowekwa moja kwa moja kwenye akaunti zao pamoja na zawadi nyinginezo.

"Kampeni ya "Twende Kidijitali, Tukuvushe Januari" ilizinduliwa katikati ya Desemba 2024 kwa lengo la kuboresha mazingira ya kibenki kwa wateja wakati wa msimu wa sikukuu na pia kuwasaidia wateja kushinda changamoto za kifedha Mwezi huu kupitia zawadi mbalimbali hivyo droo hii haitaishia hapa ni endelevu"amesema Danford

Wateja walionyesha furaha na shukrani kwa Akiba Commercial Bank kwa jitihada zake za kuimarisha huduma za kidijitali ambazo zimeboresha uzoefu wao wa kibenki kwa kuwapatia urahisi na wepesi wa kupata huduma za kifedha wakiwa mahali popote na wakati wowote
Miongoni mwa wateja akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa zawadi hizo, Bw. Alfayo Zephania alieleza jinsi alivyopokea furaha habari njema za kuibuka mshindi wa kampeni hiyo amesema "Nilifurahishwa sana na tarifa ya ushindi wangu na ninaishukuru Benki ya Akiba kwa kujali wateja wake na kutoa huduma bora na anatoa rai kwa watu wengine kujiunga na Akiba Commercial bank wanufaike na mengi ikiwemo mikopo ambayo imenivusha pakuwa katika biashara zangu”

Naye Mteja Ezekiel Willium alielezea furaha yake kwa zawadi aliyoshinda, akisema kuwa ushindi huo umempa hamasa zaidi ya kushiriki kwa bidii ili kupata zawadi kubwa zaidi katika droo kuu ya mwisho wa kampeni.

Aidha Akiba Commercial benki imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni hiyo na inawasihi waendelee kutumia huduma za kidijitali za benki .

No comments