NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS MIPANGO NA UWEKEZAJI AFUNGUA KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Kibaha - Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe Stanslaus Nyongo Leo  afungua kongamano la Biashara na Uwekezaji lilofanyika katika shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliopo Kibaha kwa Mathius na kueleza sera za Serikali katika kukuza sekta ya Biashara na Uwekezaji kwa uwanzishwaji wa Idara ya Biashara na Uwekezaji katika Halmashauri zote nchini na kuanzisha mfumo wa kusajili wawekezaji (Tanzania Investment Window).

Aidha amemshukuru Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa katika uboreshaji wa sera za Uwekezaji kwa kuanzisha Wizara maalum ya Mipango na Uwekezaji ambayo ipo chini ya Ofisi yake.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge amesema Kongamano litawezesha kujua jitihada kubwa za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika Kuboresha Sekta ya Biashara na Uwekezaji zilizotokana na Sera nzuri pamoja na utekelezaji wa Sera hizo.

Aidha Wadau mbalimbali wa Uwekezaji watapata fursa ya kuona maeneo mbalimbali ya Uwekezaji, bidhaa zinazozalishwa na kuona malighafi za viwanda zinapopatikana.

Aliongeza kuwa mdahalo huo utatumika kama njia ya kujifunza ili kuongeza spidi ya ukuwaji wa sekta ya Biashara na Uwekezaji.

Alibainisha kuwa kwa mkoa unamiundombinu Sahihi  kwa utekelezaji wa Uwekezaji zikiwemo Barabara, umeme, Maji, na gesi.

Mada zilizojadiliwa katika Kongamano hilo ni pamoja na Fursa za Uwekezaji katika uchumi wa Blue Mkoani Pwani, Matumizi Sahihi ya nishati safi  katika mabadiriko ya Tabia Nchi na Ushirikishwaji wa Sekta binafsi katika kukuza Biashara na Uwekezaji.

No comments