MBUNGE KISWAGA AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MAGU
Magu - Mbunge wa Magu, Boniventura Kiswaga (CCM) amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza malengo ya bajeti inayotengwa kila mwaka kutokana na upatikanaji wa fedha kwenye miradi ya maendeleo kama vile elimu, afya, barabara na mengine ambayo yanahitajika wilayani Magu.
Kiswaga ametoa shukrani hizo wilayani Magu leo Jumanne mbele ya waandishi wa habari baada ya kuongoza kikao cha kamati ya mfuko wa jimbo ambao unalenga kuchochea maendeleo ya wananchi
Amesema ipo miradi mbalimbali ambayo imetekeleza katika kipindi cha mwaka 2023/2024 na wananchi wamefahamishwa vema katika kitabu cha ilani ya CCM kilichozinduliwa hivi karibuni Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko.
Kitabu hicho kimechanganua namna ambavyo miradi ya maendeleo imetekelezwa katika kila kijiji kulingana na fedha za mfuko, serikali kuu na wadau mbalimbali.
“Mfuko wa jimbo tumekubaliana kupeleka fedha mahali ambapo wananchi wameanzisha kazi zao kama vile maboma ya shule za msingi, sekondari na zahanati mbalimbali ambayo yapo katika hatua ya kuezekwa.
“Tumekubaliana wataalam watakwenda kupitia vizuri ili kuona gharama halisi ya fedha ambazo zinahitajika katika kila mradi kulingana na wananchi walivyoomba. Fedha hizi zitakwenda kuleta matokeo chanya,” amesema.
No comments