JESHI LA POLISI LAWATIA MBARONI WATUHUMIWA WA TUKIO LA KUMTEKA TARIMO
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Linaendelea na oparesheni maalumu ya kuzuia vitendo vya kihalifu maeneo mbalimbali ya jiji hilo.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Kamanda kanda maalumu ya polisi Dar es salaam SACP Jumanne Murilo alipozungumza na wanahabari amesema tunaendelea na uchunguzi na kufuatilia taarifa mbalimbali na ushahidi wa kisheria kuhusiana na matukio ya kihalifu ikiwemo tukio la kutekwa kwa Mfanyabiashara Deogratius Tarimo.
Tumefanikiwa kukamata kundi la wahalifu wanane ambapo wanatuhumiwa kula njama kwa pamoja na kuweza kumteka Deogratius Tarimo.
"Watuhumiwa hao tumewakamata kwa nyakati tofauti kutoka kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo Dar es salaam, Ruvuma, na eneo la mlimba mkoani morogoro huku tumefanikiwa kukamata gari aina ya Toyota Raum ambayo ilitumiwa wakati wa kufanya tukio hilo la utekaji na ikitumia Namba isiyo halisi T 237 EGE pia tumefuatilia Namba halisi ya gari hiyo ni T237 ECF. " Amesema SACP Murilo.
Aidha Jeshi la polisi linaendelea kuzuia vitendo vya kihalifu kwani hakutokuwa na huruma kwa watuhumiwa wote ambao wanajihusisha na vitendo hivyo vya kihalifu.
Tunatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa za kweli ili Jeshi la polisi lichukuwe hatua za kisheria kwa watu wanaopanga kufanya matukio ya kihalifu ili washughulikiwe mapema kabla ya matukio
No comments