Breaking News

BENKI KUU YA TANZANIA KUZINDUA MFUMO WA MALALAMIKO WA KIDIGITALI

NA K-NEWS/KHALFAN SAID - Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kuzindua mfumo wa kidigitali utakaomuwezesha mtumiaji wa huduma za kifedha kuwasilisha malalamiko, kuanzia Januari mwaka 2025, Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Ustawi wa Huduma Jumuishi za Kifedha, BoT, Bi. Nangi Massawe amesema.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, Desemba 10, 2024, wakati akifungua warsha ya siku mbili kuhusu mfumo wa malalamiko kwa wawakilishi wa taasisi za fedha jijini Dar es Salaam.

“Mfuko umetengenezwa na kukamilika tunaamini ifikapo Januari katikati, tutauzindua rasmi ili wananchi waweze kutuma malalamiko yao, ni muhimu sana kwa kupitia warsha hii tuhakikishe wote tumeuelewa vizuri na kuanza kuutumia kabla ya kuuzindua.” Amefafanua.

Naye Kaimu Meneja Idara ya Ulinzi wa Watumiaji wa Fedha, (Financial Consumer Protection), Dkt. Hadija Kishimba, amesema BoT imeandaa warsha hiyo kwa taasisi za fedha ili kuuelewa mfumo kwani wao ndio wanaokutana na (walaji) wateja.
“Tubebe huu mfumo kwa sababu tunakwenda kusogeza huduma kwa wnanachi, tunataka mwananchi alalamike kupitia kiganja chake, alalamike kupitia computer yake.” Amesisitiza.

Amesema, “Ninyi ndio wenye mfumo, nasema hivyo kwasababu ninyi ndio mnaokutana na wananchi, BoT imeandaa mfumo na tunapopeleka automation kwenye taasisi za fedha sio lengo la BoT kubaki na mfumo huo, lengo letu wananchi watumie ili na sisi tupate mrejesho.” Amesema.

No comments