WAZIRI CHANA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAKUMBUSHO YA JIOLOJIA NGORONGORO
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ameweka jiwe la misingi la mradi wa miundombinu ya Ngorongoro Lengai Geopark wenye thamani ya takribani shilingi bilioni 25 chini ya ufadhili wa Serikali ya China ili kusaidia uboreshaji wa huduma muhimu za kitalii katika eneo hilo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uwekaji jiwe la msingi iliyofanyika Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha, leo Novemba 16, 2024 Mhe. Chana amesema ujenzi wa mradi huo ni ushuhuda wa maono ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ukuaji wa sekta ya utalii na uhifadhi wa mazingira hapa nchini.
‘‘Mradi huu utakapokamilika, utasaidia watalii na wakazi wa wilaya za Ngorongoro, Karatu, Monduli, na Longido kunufaika kutokana na kuboreshwa kwa huduma za mawasiliano, nyumba ya kumbukumbu, na tafiti za kisayansi.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingian amesema Serikali ya China itaendeleza mahusiano yaliyopo baina ya Mataifa hayo Mawili ikiwemo kuboresha sekta ya utalii kuunga Mkono sera ya Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukuza utalii kupitia filamu mbali mbali.
‘‘Ushirikiano kati ya Tanzania na China umeimarika vya kutosha na niwahakikishie kuwa Serikali ya China itaendelea kushirikiana katika maendeleo ya sekta ya utalii" amesema Mhe. Chen.
Naye, Katibu Mtendaji wa UNESCO nchini Tanzania Prof. Hamis Malebo amesema hifadhi ya Miamba ya Ngorongoro ndio hifadhi kubwa na yenye maajabu makubwa Barani Afrikka kutokana na uwepo wa Kreta mbili za ajabu na volcano hai.
Kwa hali hiyo Tanzania ina maajabu makubwa Sanaa ambayo yanapatikana hapa tu, nipende pia kuishukuru UNESCO kwa kuendelea kuisaidia hifadhi ya Miamba ya Oldonyo Lengai ambayo mpaka sasa imeweza kuboresha mambo makubwa sana’’ amesema Malebo.
Wizara ya Maliasili na Utalii hadi kufikia Mei, 2024 Idadi ya watalii imefikia asilimia 96 ambapo kukamilika kwa mradi wa Makumbusho ya Jiolojia ya Ngorongoro-Lengai itapelekea kukuza zaidi sekta ya utalii, ongezeko la ajira na kukuza uchumi
No comments