Breaking News

TMA YATANGAZA MVUA KUBWA MIKOA 11 KUANZIA LEO NOV 30, 2024

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetabiri mvua kubwa kwa siku mbili kuanzia leo Novemba 30 na Desemba mosi, mikoa 11 kwenye kanda tatu tofauti.

Utabiri huo, mbali na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe na Rukwa), umegusa ukanda wa Pwani ya Kusini mwa Bahari ya Hindi (Lindi na Mtwara), Kanda ya Kati (Dodoma na Singida) na Kanda ya Kusini mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Morogoro.

“Angalizo la mvua kubwa kwa maeneo machache ya Nyanda za juu Kusini Magharibi mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa na Songwe, Ukanda wa Pwani ya Kusini mwa bahari ya Hindi mikoa ya Lindi na Mtwara, Kanda ya Kati mikoa ya Dodoma na Singida na Kanda ya Kusini (mkoa wa Ruvuma) na mkoa wa Morogoro,” imesema taarifa ya TMA.

No comments