Breaking News

MBUNGE TURKY ATETA NA SPIKA WA COMORO

Mbunge wa Jimbo la Mpendae Mheshimiwa, Toufiq Turky amekutana na Spika wa Bunge la Comoro Mheshimiwa Moustadroine Abdou ambapo wamezungumzia ushirikiano wa Tanzania na Comoro katika eneo la uwekezaji.

Mheshimiwa Turky ambae amewekeza katika miradi kadhaa nchini Comoro alimueleza mipango yake kwa hivi sasa hususan katika eneo la ujenzi wa hoteli ya kisasa. Aidha, Mheshimiwa Turky alipongeza hatua ya Comoro kujiunga na Shirika la Biashara Duniani (WTO) hatua inatosaidia kujenga zaidi imani kwa wawekezaji wa nje.
Kwa upande wake Spika Moustadroine alimueleza Mheshimiwa Turky namna Tanzania na Comoro zilivyo na uhusiano wa karibu wa kihistoris na kuwa hivi karibuni Bunge la nchi hiyo limetunga sheria kadhaa za kulinda wawekezaji.

Mheshimiwa Toufiq ambaye pia ni Mwakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mheshimiwa Said Yakubu katika mkutano huo ulioratibiwa na Ubalozi.

No comments