Breaking News

WAZIRI LUKUVI AWAPA TANO VIONGOZI WA CHAMA CHA NLD

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. William Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa chama cha NLD wakati akihitimisha ziara yake makao makuu ya Chama hicho yaliyopo Tandika, Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. William Lukuvi, akizungumza makao makuu ya chama cha NLD mapema leo 8 Oktoba 2024 wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili kutembelea katika ofisi za Vyama vyenye usajili wa kudumu Tandika Jijini Dar es Salaam

Dar es salaam,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. William Lukuvi, leo tarehe 8 Oktoba 2024 amefanya ziara katika ofisi za Chama cha NLD zilizopo Tandika, Jijini Dar es Salaam. 

Katika ziara hiyo, Mhe. Lukuvi aliambatana na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mtungi. Mhe. Lukuvi alikutana na Mwenyekiti wa chama hicho, Mhe. Mfaume Khamis, pamoja na viongozi mbalimbali ikiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Doyo Hassan Doyo na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Khamis Said Hamad, sambamba na Makamu Mwenyekiti Bara, Mhe. Othiniel Mizizi.
Mhe. Lukuvi aliwapongeza watendaji wa Chama cha NLD kwa msimamo wao mzuri unaombea uzalendo na uvumilivu, akisisitiza umuhimu wa uzalendo katika kazi za kisiasa. Aliongeza kuwa ni muhimu kwa viongozi wa Chama cha NLD kuwashawishi wanachama wao kujitokeza kujindikisha na kupiga kura, kwani ni haki yao ya kikatiba, Mhe Lukuvi alisema, "Tumekuwa tukisikia matamshi yenu; NLD ni chama cha demokrasia kinachobeba haki na uzalendo."

Aidha, Mhe. Lukuvi alieleza matamanio yake ya kusikia sera nzuri za NLD wakati wa kampeni zitakazoanza, akionyesha imani kwa NLD, kuwa kitatoa maono ya kipekee katika kipindi cha uchaguzi wa serikali ya mtaa, vijiji na vitongoji na hatimaye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025

No comments