Breaking News

WAZIRI CHANA AFUNGUA SHULE YA MSINGI YA NAMLANGWA ILIYOGHARIMU MIL 638

Kalambo - Rukwa 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amefungua shule ya Msingi Namlangwa iliyojengwa kwa fedha takribani shilingi milioni 638.5, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa leo Oktoba 1,2024.

Ujenzi wa mradi huo ulijumuisha vyumba viwili vya elimu ya awali, vyumba 14 vya Elimu Msingi, matundu 24 ya vyoo na kichomea taka.

Akizungumza baada ya kufungua shule hiyo, Mhe. Chana ametoa rai kwa Maafisa elimu na Serikali za Vijiji kufuatilia takwimu za wanafunzi wanaopaswa kwenda shule na kuwarejesha ambao hawako shule.
"Urithi pekee unaoweza kumpa mtoto ni elimu, tunataka taifa ambalo limeelimika na lenye nguvu kazi ya kutosha" amesisitiza Mhe. Chana.

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha watanzania wanapata elimu bure na bora.

Awali, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Mkuu wa Shule ya Msingi Namlangwa, Enock Elly ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha za mradi wa BOOST ambazo zimesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuongeza ufanisi wa walimu katika kutelekeza majukumu yao.





No comments