WATAALAMU SEKTA YA UJENZI WAZAWA WATAKIWA KUWA NA USHIRIKINO KATIKA KUFANYA KAZI - DC MPOGOLO
Wataalamu wa Sekta ya ujenzi ikiwemo wabunifu wa majengo, wakadiriaji na wakandarasi wa ndani ya nchi wapewe kipaumbele kupata fursa.
Akizungumza katika mkutano Mkuu wa 5 wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu na Wakadiriaji Majengo (Architects and Quantity Surveyors Registration Board), Jijini Dar es kwenye katika ukumbi wa Julius International Convention Center.
Katika mkutano huo ambapo uliowakutanisha viongozi wa Serikali, wahitimu wa vyuo vya elimu sekta ya ujenzi, Viongozi wa dini, wasanifu majengo na wakandarasi, Watumishi Bodi ya Usajili wa Wabunifu na Wakadiriaji majengo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema wataalamu wa ndani wanaweza kufanya kazi imekuwa ni kawaida wadau wa ndani huwaita wataalamu wa nje kufanya kazi badala ya kushirikisha wazawa kupata fursa, hivyo inatakiwa wataalamu wa nje washirikiane na watalamu wa ndani kutekeleza miradi ya ujenzi.
"Amesema wazawa wanauwezo wa kufanya kazi ila wanatafuta wageni ili waweze kugawana pesa badala kutafuta wazawa wenzake" alisema Mpogolo.
Pia amesema inatakiwa Watanzania wawe wazalendo katika kufanya shughuli za kutelekeleza miradi mbalimbali ya Serikali na sekta binafsi kufanya kazi kwa weledi na ustadi mkubwa kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Aidha amewataka wataalamu kujenga umoja na mshikamano wazawa kwa wazawa ili kuweza kupata kazi kwa pamoja.
Kadhalika mhe. Mpogolo amewataka wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari kupenda masomo ya sayansi ili kupata wataalamu wengi wa usajili wa wakadiliaji wa majengo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa wabunifu na Wakadiriaji wa Majengo (Architects and Quantity Surveyors Registration Board) Dkt. Ludigija Bulamile amesema kuna ongezeko la wabunifu majengo wenye ustadi na ubunifu mkubwa katika kuleta matokeo chanya, lakini pia wamekuwa na juhudi katika kuwatafuta wahitimu na kuwapatia mafunzo na wamefanikiwa kuwapatia elimu watihimu katika sekta hiyo.
Aidha wataalamu waliohitimu siku ya Leo ni wataalam 165
Kwa upande wake mwakilishi wa katibu mkuu wizara ya ujenzi Daudi Kandoro amesema wizara itaendelea kusimamia mabadiliko chanya ili kuwawezesha wakandarasi kupata mafunzo.
Amesema wizara ya ujenzi ipo katika kuandaa Sheria za wabunifu wa majengo.
No comments