Breaking News

WAKILI DKT. HAMIS - ATOA WITO KWA SERIKALI KIHESHIMU HAKI ZA BINADAMU

Serikali na Taasisi zake zote zinazosimamia masuala utoaji wa haki wametakiwa kuhakikisha wanalinda na kufuata Sheria na miongozo ya haki za binadamu.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mdau wa haki za binadamu kutoka Taasisi ya Everlasting Legal Aid Foundation wakili Dokta Hamis Masoud juu ya tuhuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikiripotiwa na vyombo vya habari pamoja na jamii juu ya uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa na baadhi ya maofisa wa polisi pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.

Dokta Hamisi amesema katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na taarifa na tuhuma mbalimbali wanazokuwa wakizipokea wao kama wadau wa haki za binadamu kutoka kwa jamii wakililalamikia juu ya utendaji Jeshi la Polisi kupitia baadhi ya maofisa wake kukiuka utaratibu wa kisheria wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.

Baadhi yao wamekuwa wakiteka watu, kunyanyasa na Kuminya haki za watu akitolea mfano tukio la hivi karibuni la ukatili na unyanyasaji wa binti kutoka kwa baadhi ya Ofisa wa Polisi.

Alisema hili kuhakikisha kuwa kunakuwepo na usawa na ufutaji wa sheria ni vizuri Jeshi la polisi linapochunguza tuhuma yoyote ya Ofisa liwe na uwazi na pale litakapo bainika kosa mtuhumiwa achukuliwe hatua za haraka.

"Nitoe wito kwa Jeshi la Polisi kuweka mifumo mizuri ambayo itasaidia pindi watakapotokea baadhi yao kutokuwa waadilifu kuweza kuwajibishana wao kwa wao kwa kulingana na ngazi ya vyeo hii itasaidia kurejesha imani kwa jamii kwa Jeshi Hilo juu ya uhuru, ulinzi na usalama wao". Alisema Dkt. Hamis

Katika hatua nyingine Dkt. Hamisi amesisitiza Maofisa wa Jeshi la polisi kusimamia sheria pindi watekelezapo majukumu yao hususani waandishi wa habari pindi wanapokuwa wakifanya kazi zao za kitaaluma kwa mujibu wa sheria na haki ya mwananchi kupata habari.

No comments