Breaking News

VIONGOZI WA NCHI ZA SADC KUKUTANA DAR, KUJADILIANA NAMNA BORA YA KUFUFUA VYANZO VYA NISHATI

Katibu Mkuu anayeshughulikia Umeme, Dkt Khatibu Kazungu akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Wanachama Jumuiya ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) kujadili mikakati endelevu ya kufufua vyanzo vya nishati pamoja na changamoto walizonazo ili waweze kuzitatua jijini Dar es Salaam
Naibu Mkurugenzi Mtendaji uzalisahi umeme TANESCO, Mhandisi Costa Rubagumya akifafanua jambo mkutano Wanachama Jumuiya ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) kujadili mikakati endelevu ya kufufua vyanzo vya nishati pamoja na changamoto walizonazo ili waweze kuzitatua jijini Dar es Salaam.

Dar es salaam;
Wanachama wa Jumuiya za Nchi Kusini Mwa Afrika (SADC), wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili mikakati endelevu ya kufufua vyanzo vya nishati pamoja na changamoto walizonazo ili waweze kuzitatua.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu anayeshughulikia Umeme, Dkt Khatibu Kazungu , amesema wataalamu wa umeme kutoka Jumuia hiyo wamekutana kwa lengo la kujadili na kutatua changamoto wanazokutananazo ili wafikie malengo mahususi hiyo kwa lengo la kufanikisha kusafirisha na kusambaza kwa wateja wa ukanda huo.

"Lengo la mkutano huu wa wataalamu wa umeme wa Jumuia ya SADC ni kuweka mikakati madhubuti ya kutumia vyanzo vilivyopo ili kushirikiana kwa pamoja katika kufufua umeme, kusafirisha na kusambaza kwa wateja.

“Sisi kama Serikali tuna mradi unaoitwa TAZA, wenye lengo la kuunganisha miundombinu ya umeme hapa Tanzania na Zambia na tunapokutana katika vikao kama hivi tunapitia mikakati hiyo na hatua ambayo tumefikia na kutua changamoto zinazotukwamisha kufikia malengo hayo, ” amesema.

Pia ameongeza kuwa, mahitaji ya umeme wa ndani huko vizuri kutokana na kuwepo kwa mradi wa Bwawa la Nyerere ambalo kwa sasa linauwezo wa kuzalisha megawati 700 na siku chache zijazo litazalisha megawati 900.

Amebainisha kwamba tofauti na Bwawa la Nyerere pia kuna vyanzo vingine kikiwemo cha mradi wa Umeme wa Jua, ambao kwa sasa una uwezo wa kuzalisha megawati 600 na kupitia Joto Ardhi nako kunazalishwa umeme megawati 5000 na kufanya Tanzania isiwe na tatizo la uzalishaji wa umeme na kinachotakiwa ni kujipanga vizuri kama Serikali kuongeza vyanzo vingine.

“Serikali pia ina mradi mwingine wa umeme unaoitwa Green Imara ambao ni mahususi katika kuboresha miundombinu ya umeme na kuingeza vyanzo vingine na kuunganisha nishati hiyo katika mikoa ya pembezo mwa nchi ambayo Katavi, Kigoma, Lindi na Mtwara hadi mwisho wa mwaka huu itakuwa imeeinguzwa katika gridi ya Taifa,” amesema.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji uzalisahi umeme TANESCO, Mhandisi Costa Rubagumya, amesema Tanzania iko katikati ya ‘East Africa Powe Pool’ ambako inapatikana Kenya na kwa upande wa ‘Southern African Power Pool’ inapatikana Zambia.

“Katika maeneo hayo mawili inatupa uwezekano wa kusaidiana katika nyanja ya umeme ikiwa nchi mojawapo inapokuwa na shida ya nishati hiyo, mfano eneo la Kariba kwa sasa lina ukame na kusababisha Zimbabwe na Zambia kupitia katika kipindi kigumu na kutokana na kuwepo kwa ushirikiano huu unatoa fursa ya kusaidiana na kutuweka salama katika nyanja ya umeme,” amesema. 

No comments