Breaking News

TANZANIA KUADHIMISHA SIKU YA MBOLEA DUNIANI OKTOBA 13 MKOANI MANYARA.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania ( TFRA) Joel Laurent akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa juu ya maadhimisho ya siku ya mbolea duniani ambayo yatafanyika Oktoba 13 mkoani Manyara.

Dar es salaam 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara mheshimiwa Queen Sendiga anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kuadhimisho ya siku ya Mbolea Duniani yatakayofanyika Oktoba 13 , 2024 mkoani humo.

Akizungumza jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania ( TFRA), Bwana Joel Laurent amesema maadhimisho hayo nchini yanadhimishwa mara sita ambapo kwa mara ya kwanza yalifanyika Mkoani Katavi Mwaka 2019, Mwaka huu yatafanyika Mkoani Manyara kuanzia Oktoba 10 hadi 13 na yatafunguliwa na Mkuu wa Mkoa huo Mh. Queen Sendiga na siku ya kilele mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe.

Amesema maadhimisho hayo ni mpango wa Kimataifa unaoungwa mkono na Jumuiya za tasnia ya Mbolea Duniani kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu faida na matumizi sahihi ya Mbolea na kuchochea juhudi za ubunifu katika teknolojia za Kilimo kwa mustakabali wa Maendeleo endelevu ya usalama wa Chakula.

Amesema kwamba katika maadhimisho hayo wataalamu mbalimbali kutoka Taasisi za utafiti, Kampuni za Mbolea, vyuo vikuu, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na wadau wa Kilimo watapata fursa ya kutoa Elimu kwa wakulima ikiwemo Elimu ya matumizi sahihi ya Mbolea,matumizi ya mbegu Bora na udhibiti wa Tasnia ya Mbolea kwa ujumla". Alisema bw. Laurent

Alisema kuanzia tarehe 8 hadi 12 wakulima watapata fursa ya kujifunza kwa vitendo katika mashamba ya mfano yaliyoandaliwa na Mamlaka na kujionea tofauti kati ya mazao yaliyotumia Mbolea na ambayo hayajatumia Mbolea na hivyo Kuwapa hamasa au ushawishi wa kutumia Mbolea ili kuongeza tija katika uzalishaji.

Bwana Laurent aliongeza kuw amaadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani mwaka huu yamepewa mbiu "Tuongee Mbolea, Kilimo ni Mbolea," lengo ni kuonesha umuhimu wa Mbolea kama kichocheo Cha uzalishaji wa mazao ya Chakula, Biashara, mboga mboga na matunda kuongeza ukuaji wa tasnia ya Mbolea unaendelea kuchochea Kilimo Biashara kutokana na ongezeko la matumizi sahihi ya Mbolea.

Alisema kauli mbiu hiyo inakuwa kufatia juhudi za serikali chini ya uongozi wa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kuthamini umuhimu wa Mbolea katika Sekta ya Kilimo ambapo kwa misimu mitatu mfululizo Serikali imeendelea kuwanufaisha Wakulima kwa kuweka Ruzuku kwenye Mbolea mbango ambao umeongeza hamasa ya matumizi ya Mbolea kwa Wakulima na kuchochea na kuongeza tija katika uzalishaji.

"Katika maadhimisho ya Mwaka huu mamlaka (TFRA) imeandaa Kongamano la aina yake la Kimataifa la Kwanza la Mbolea litakalofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma Oktoba 11 na 12 ambalo litawakutanisha Wadau zaidi ya 250 wa tasnia ya Mbolea Kitaifa na Kimataifa kujadiliana na kuja na majibu ya changamoto zinazoikabili tasnia ya Mbolea na wakulima kwa ujumla, Kongamano hilo litaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara y Kilimo bwana Gerald Mweli.

"Katika Kongamano hilo washiriki kutoka ndani na nje ya nchi watoata wasaa wa kujadiliana pamoja na wasimamizi thabiti wa Mbolea, Tathmini ya mifumo na udhibiti Bora wa Mbolea, mchango wa Afya ya udongo katika kusimamia usalama wa Chakula Nchini.

Amezitaja mada zingine KUWA ni pamoja na matumizi ya Tehama katika kusimaia Tasnia ya Mbolea, kuhamasisha uzalishaji wa ndani, matumizi sahihi ya Mbolea na Biashara ya Mbolea katika Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusaini mwa Afrika ( SADC).

Nae Kaimu Mkurugenzi uzalishaji wa ndani na ununuzi wa Mbolea kwa pamoja Bwana Louis Kasera amesema kwasasa matumizi ya Mbolea yamefikia kiasi cha tani laki nane na arobaini kwa mwaka ukilinganisha na tani laki tatu na sitini Mwaka 2021/2022 kipindi ambacho mpango wa utoaji wa Mbolea ya ruzuku ukianzishwa na Rais Dkt Samia.

"Matumizi ya Mbolea yamepanda kutokana na wakulima wengi kuanza kuhamasiaka kutumia Mbolea ya ruzuku kwa usahihi zaidi katika maeneo mbalimbali Nchini". Alisema Kasera.

No comments