Breaking News

SEKTA YA UTALII INATOA MCHANGO MKUBWA WA AJIRA NA PATO LA TAIFA - NAIBU WAZIRI KITANGULA

Neema Mpaka, Dar es salaam
Naibu waziri wa wizara ya Mali asili na utalii Mh Dunstan Kitandula amesema sekta ya utalii imekuwa na mchango mkubwa kwenye ajira za watanzania na kuchangia Pato la taifa.

Ameyasema hayo Leo jijini dare es salaam wakati wa mkutano wa jukwaa la kitaifa la wawekezaji kupitia utalii ,ambalo limefanyika Leo octoba 12,2024 sambamba na onesho la kiswahili international Tourism Expo (S!TE) katika ukumbi wa mlimani city.

Aidha amesema hayo ni matokeo ya juhudi za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kufungua utalii kwa kutangaza vivutio hpa nchini ambapo imepelekea ongezeko la watalii.

"Mkutano huu ni muhimu sna Kwani umehusisha watu wa wanaotaka kuwekeza katika sekta ya utalii ikiwemo mahotel na kujadili fursa zilizopo nchini Amesema "

Amesema kupitia mkutano huo wawekezaji katika sekta ya utalii kando ya onesho la S!TE 2024 inadhiirisha na kuwaaminisha wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania kuwa Tanzania ni sehemu salama kuwekeza ambapo asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni hapa nchini huchangiwa na sekta ya utalii.

"Amesema Tanzania ni eneo salama la kuwekeza ambalo linawapa uhakika wa kufanya biashara inayohitajika na wakapata faida" Amesema.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa bodi ya utalii Tanzania (TTB) Balozi Ephraim Mafuru amesema kwa mwaka huu kupitia onesho la S!TE kama moja ya mazao ya utalii limezidi kuitangaza vyema Tanzania kimataifa hivyo limepelekea kupata washiriki wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali Dunia.

"Mwaka huu washiriki wote walioshiriki katika onesho hili kubwa la kimataifa la utalii barani Afrika la S!TE 2024 watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali ya utalii hapa nchini ili kujionea mazuri tuliyobarikiwa kama taifa kupitia utalii"

Alikadhalika Balozi Mafuru wamewakaribisha watanzania na wasio watanzania kuendelea kuwekeza katika sekta ya utalii.

Amesema sekta hii ya utalii imekuwa ni miongoni mwa sekta zenye mafanikio makubwa kutokana na kuzidi kukua mwaka hadi mwaka jambo lililoiweka Tanzania katika ramani nzuri ya utalii kimataifa kupitia vivutio vyake.

No comments