PICHA: MAFUNZO KONGAMANO LA JOTOARDHI AFRIKA LINALOENDELEA JIJINI DAR ES SALAAM
Washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani wakiwa katika mafunzo yanayofanyika kwenye Kongamano la Kimataifa la Jotoardhi (ARGeo - C10) linaloendelea jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yanahusu masuala mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati ya Jotoardhi, uhandisi wa visima vya Jotoardhi na teknolojia mpya, njia za kupata ufadhili wa miradi ya nishati mbadala ikiwemo jotoardhi na uchambuzi wa faida za kimazingira na kijamii katika maendeleo ya miradi ya jotoardhi.
No comments