CCM IMERIDHISHWA NA TAKWIMU ZA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA WAKAAZI LA WAPIGA KURA
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makalla na Mlezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam amezungumza hayo wakati wa hafla ya kupokea taarifa ya zoezi la uandikishaji wa daftari la mkazi la uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mkoa wa Dar es Salaam, taarifa aliyoipokea kutoka kwa viongozi wa CCM wa mkoa huo leo, Jumanne Oktoba 22.2024
Nianze kuwapongeza Viongozi wa CCM kuanzia ngazi Mkoa mpaka Mabalozi pamoja na Wafuasi wa CCM na Wananchi kwa Ujumla yaani Mkoa mzima wa Dar es salam kwa kutoa Ushirikiano katika zoezi zima la Uandikishaji mpaka kufikia asilimia 96.7 hii ni faraja kwa CCM kwani Dar es salam ni uso wa Nchi.
Awamu hii Wananchi wamejiandikisha kwa wingi sana na hii imechagizwa na Utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM hilo halina kificho kwa sababu miradi haitekelezwi hewani,Miradi ya Zahanati, Madarasa,Vituo vya Afya imetekelezwa kwenye Vijiji na Vitongoji hivyo Wananchi wameona kazi ya Dkt Samia Suluhu Hassan
CPA Makalla amesema endapo chama hicho tawala hapa nchini kitapoteza kwenye baadhi ya vitongoji, vijiji au mitaa vitaheshimu matokeo hayo na kwamba huo utakuwa wakati muafaka kwao kujitafakari na kujipanga kwa nini walipoteza eneo hilo, ili uwe njia ya kufanya vizuri kwenye uchaguzi ujao
Mwisho Mwenezi Makalla amesisitiza CCM haihitaji mbeleko kwani kwa takwimu tulizopokea ndani ya Chama na zile za Wizara ya Tamisemi kwani Maandalizi yaliyofanyika na Viongozi wa CCM wote na Jumuiya Kwa kazi nzuri na kuleta taswira ya Ushindi wa kishindo.
No comments