Breaking News

MWENYEKITI WA BODI NCAA ATEMBELEA ONESHO LA SITE 2024 NA KUPONGEZA JUHUDI ZA KUTANGAZA UTALII.

Na Hamis Dambaya, NCAA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu) ametembelea banda la mamlaka hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Swahili International Tourism Expo 2024 yanayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar esalaam na kuipongeza menejimenti kwa kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa katika kuendeleza uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.

Katika banda la NCAA mwenyekiti huyo wa bodi alipokea maelezo ya ushiriki wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika maonesho hayo kutoka kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi anayeshughulikia huduma za utalii na Masoko Bi Mariam Kobelo ambapo alisema kuwa ushiriki wa maonesho hayo unasaidia kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kufanya utalii katika hifadhi hiyo.
Bi Kobelo amesema kuwa wageni wengi wanaofika katika banda hilo hupata nafasi ya kuelezwa vivutio mbalimbali vilivyopo katika hifadhi ya Ngorongoro ambapo wageni wanaotembelea hifadhi hiyo wanaona wanyama mbalimbali kama vile samba, tembo, chui,faru,nyati,swala,twiga na wengine lakini pia hipata nafasi ua kujua historia ya binadamu kupitia makumbusho ya Olduvai Gorge, kuona mchanga unaohama, nyayo za zamadam na vinginevyo vingi.

"NCAA tutaendelea kutumia maonesho mbalimbali katika kujitangaza na njia hii imekuwa ikisaidia kuongeza wigo wa watalii wa ndani na wa kimataifa jambo ambalo limesaidia sana pia kuongezeka kwa idadi ya wageni wanaotembelea hifadhi hiyo” aliongeza Kobelo.

Onesho ya kimataifa ya SITE huwakutanisha wadau wa sekta ya utalii kutoka ndani na nje ya nchi ambapo pamoja na mambo mengine husaidia kukuza utangazaji wa utalii ambapo wadau mbalimbali hukutana kwa pamoja chini ya Mwamvuli wa wizara ya Maliasili na Utalii.

No comments