Breaking News

HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA YATOA MAFUNZO KWA WAANDIKISHAJI WAPIGA KURA NGAZI YA VITONGOJI

Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tarehe 08/10/2024 inatoa mafunzo kwa Waandikishaji wa Orodha ya wapiga kura ngazi ya Vitongoji, watakaotekeleza zoezi la uandikishaji wapiga kura linalotarajia kuanza tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024.

Mafunzo ni ya siku mbili yanayofanyika makao makuu ya Tarafa katika Tarafa tatu za Ruhekei, Mpepo na Ruhuhu yameanza leo Oktoba 08, 2024 na yatakamilika Oktoba 09/2024 kwa washiriki kutoka Kata 20 za Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza Majukumu Yao.

Akifungua mafunzo kwa niaba ya Msimamizi wa uchaguzi, Mjumbe wa Sekretarieti ya Uchaguzi Bw.Shabanho Mwaipopo amewataka washiriki, kuzingatia Sheria, Kanuni, miongozo na maelekezo ya Serikali katika zoezi hilo ili kufikia lengo la kuandikisha watu wote wenye sifa za kupiga kura.
Aidha, amewataka kusikiliza kwa makini wakati wawezeshaji wakiwasilisha mada mbalimbali kuhusu zoezi la uandikishaji ili waweze kufahamu sifa na utaratibu wa kuwaandikisha wapiga kura.

“Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Nyasa hategemei kusikia mtu ameharibu kazi kwa uzembe wake na badala yake kazi ikamilike vizuri kwa mujibu wa sheria za nchi” .





No comments