Breaking News

MAMA MARIAM MWINYI KUSHIRIKI MKUTANO WA MECK FOUNDATION

Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mhe. Mama Mariam Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili jijini Dar es Salaam.

Mama Mariam Mwinyi atashiriki Mkutano wa 11 wa Merck Foundation Africa Asia Luminary utakaofanyika tarehe 29 - 30 Oktoba 2024 katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 700 kutoka Mataifa mbalimbali duniani, ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mkutano huu unalenga kujadili na kutafuta suluhu dhidi ya changamoto mbalimbali za afya na kijamii zinazokabili bara la Afrika na Asia.


No comments