Breaking News

BRELA YASHIRIKI MAONESHO YA MADINI GEITA

Wakala wa Usajili wa Leseni (BRELA) wamesema kuwa wapo katika maonyesho ya madini mkoani Geita Kwa lengo ya kuwafikia wadau na kutoa huduma za papo Kwa papo kama kusajili Majina ya biashara, Kampuni na leseni za viwandani.

Pia wamesema lengo la kushiriki ni kuweza kukutana na wadau muhimu ambao ni wafanyabiashara wa madini na wafanyabiashara wengine Kwa ujumla .

Kauli hiyo imetolewa Octoba 5, 2024 na Afisa leseni Mwandamizi bwana Koyan Aboubakar katika maonyesho ya Saba ya kimataifa ya Teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya bombambili vilivyopo Mjini Gaita.

Ameongeza kuwa wamekuja mkoani Geita katika mkusanyiko huo Kwa ajili ya kutoa huduma za papo Kwa papo na kutoa elimu ya huduma zinazotolewa Brela na Kwa wale ambao wanataji kupata huduma, huduma zote zinaweza kukamilika kwenye Banda la Brela lililopo kwenye viwanja vya maonyesho Mjini humo.

"Kitu cha msingi niwatake wananchi wa Geita na mikoa ya jirani kujitokeza Kwa wangi ili kutatua changamoto zao na hasa kwenye eneo la usajili 

"huduma zinatolewa hapa na zitakamilika hapahapa na dhamira ya kuja kushiriki maonyesho haya nikuwafikia wadau Wetu ambao wapo hapa Kwa wingi na wamekuja Kwa ajili ya kutanga bidhaa zao na sisi tupo Kwa ajili ya kusajili ."amesisitiza Aboubakar

No comments