Breaking News

UMOJA WA WANAWAKE WASAFIRISHAJI STENDI YA MAGUFULI WAPATIWA MAFUNZO YA UKATILI WA KIJINSIA,

Afisa Maendeleo ya jamii wilaya ya ubungo - Kibamba, Bi. Beatrice Mbawala akizungumza katika ufunguzi warsha ya siku moja ya haki za kijinsia iliyowakutanisha makundi ya wanawake na wadau wa usafirishaji Magufuli bus terminal.
Mwenyekiti wa (UWAM) Bwana Peter Ndengerio akielezea namna warsha hiyo ya siku moja itavyosaidia utekelezaji wa majukumu yao.
Mratibu wa Mradi wa Haki za wanawake a watoto katika sekta ya usafirishaji abiria Magufuli bus terminal, Bi. Dahlia Majid akielezea mradi huo wakati akiwasilisha mada katika warsha hiyo ya siku moja.

Dar es salaam 
Umoja wa Wasafirishaji Abiria Mikoani (UWAM) umetoa warsha ya siku moja kwa wanachama wake ikiwa ni awamu ya pili kuhusu mradi wa haki za Wanawake na Watoto katika Sekta ya Usafirishaji Magufuli Bus Terminal (Mafuli Bus Terminal Awamu ya Pili)

Akizungumza katika ufunguzi wa warsha hiyo Afisa Maendeleo ya jamii wilaya ya ubungo - Kibamba, Bi. Beatrice Mbawala amesema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo pamoja na kubadilishana mbinu kitendo cha kuwa mwanamke au mtoto kinavutia kuwa chanzo cha kupata changamoto ya utalii.

"Serikali ipo tayari kupokea changamoto zeni na kuweka Mpango mkakati wa kuzitatua hili kuboresha Mazingira na kuwezesha kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi zaidi". Alisema Bi. Mbawala.

Alisema washriki wa warsha hiyo ni vema pia kubainisha changamoto zao na kuweka wazi ili Serikali iweze kuzishughulikia na kuzipatia ufumbuzi.

Pia alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi hususani wa mikoani kutoruhusu watato wao kuja Dar es Salaam kuyokana na wengi wao kudanganywa kwa ajira jambo ambalo linawafanya watoto waishie katika vitendo vya ukatili.

Pia bi. Mbalawa ametoa wito kwao kuwa na utaratibu wa kufanya operesheni za mara Kwa mara katika kituo hicho pamoja na kiwasaidia waanga wa matukio hayo kiwarudisha watoto nyumbani kwao Mikoani walikotokea.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa (UWAM) Bwana Peter Ndengerio akielezea mradi huo amesema umelenga kushughuolikia changamoto mbalimbali ikiwemo ya vyoo, lugha za matusi ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo hususani Wanawake na Watoto katika kituo hicho. 

Naye Mratibu wa Mradi wa Haki za wanawake a watoto katika sekta ya usafirishaji abiria Magufuli bus terminal, Bi. Dahlia Majid amesema mradi huo umelenga Wanawake na Watoto hususani waliopo eneo la Magufuli Bus Terminal.

Washiriki wa warsha hiyo ya siku moja ni Makundi ya Wanawake Mawakala wa Mabasi, Mama Lishe, Wauza Vinywaji na Wabeba Mizigo.


 

No comments