Breaking News

DENI LA SERIKALI YA TANZANIA LAFIKIA TRILIONI 98

Ripoti ya mwezi ya Benki ya Tanzania inaonesha mpaka Julai 2024, deni la serikali lilifikia Trilioni 98.5 huku asilimia 67 ya deni hilo likiwa ni deni la nje sawa na dola za kimarekani Bilioni 24.69, ambazo ni Trilioni 66 za Kitanzania.

Sekta iliyopokea mikopo mingi ni usafirishaji na mawasiliano ambapo ilipokea asilimia 25.9 ya mikopo yote ikifuatiwa na huduma za kijamii na mawasiliano iliyopokea asilimia 23.9 ya mkopo wote.

Kati ya mwaka 2020 na mwaka 2024, deni la ndani limeongezeka mara mbili kutoka Trilioni 15.1 mwaka 2020 mpaka kufikia Trilioni 32 mwaka 2024. Wakopeshaji wakubwa wa ndani ni Benki za Kibiashara (30.2%), Mifuko ya Hifadhi (27%), Benki Kuu( 23%), Kampuni za Bima (5.7%) na nyinginezo (14%).

Source The Chanzo

No comments